Chia
seeds ni mojawapo ya vyakula vyenye kiwango kikubwa cha
virutubisho.Mbegu za chia zina virutubisho mbali mbali ambavyo ni muhimu
kwa afya ya mwili na ubongo. Mwili ni rahisi kupata virutubisho vyote
vilivyomo katika mbegu hizi kwani zinameng'enywa kwa urahisi sana.
HISTORIA YA CHIA SEEDS
Mbegu
hizi zinatokana na mmea unaojulikana kitaalam kama SALVIA HISPANICA,
mmea huu unapatika sana Amerika ya kusini japo siku za hivi karibuni zao
hili linalimwa hapa nchini Tanzania mikoa ya Morogoro na
Karagwe(Kagera).
Mbegu
hizi tokea zamani zimekua zikitumiwa kama chakula na dawa ya magonjwa
mbalimbali na makabila ya AZTECS na Mayans yote kutoka Amerika ya
kusini. Chia ni neno la Lugha ya Wa AZTEC likiwa na maana ya nguvu.
Inasemekana kwamba kijiko kimoja cha mbegu za chia zilikuwa zinaweza
kuwafanya watu kukaa masaa 24 bila kuhitaji chakula kingine,hivyo zao
hili lilikua likitumika sana kwa askari ili kuwasaidia kuwapa nguvu na
kustahimili magonjwa mbali mbali.
VIRUTUBISHO VILIVYO NDANI YA MBEGU ZA CHIA
Sababu
ya mbegu kuwa na umuhimu katika afya ya mwili ni kutokana na kiwango
kikubwa cha virutubisho vilivyomo ndani yake. Mbegu hizi zina kiwango
kikubwa cha omega- 3, Vitamini,proteini na madini.
Gram 28 za chia zinakua na virutubisho katika kiwango kifuatacho
FIBER- 39 gm
PROTINI- 14 gm
MAFUTA- 32GM (18 gm ikiwa ni Omega 3, na 6gm Omega 6)
MADINI KWA KIWANGO KINACHOHITAJIKA KWA SIKU
Calcium- 64%
Manganese- 107%
Magnesium-107%
Phosphorous - 96%
Pia mbegu hizi zina Vitamin A,B,D na E, Madini joto kama Iron,Iodine,niacine, thymine na kemikali za kulinda mwili ( antoxidants)
FAIDA ZA CHIA SEEDS KIAFYA
Tafiti
zinaonesa kwamba unapotumia mbegu hizi mara kwa mara inaweza kuimarisha
afya ya mwili wako na kukukinga na magonjwa mbalimbali.
Zifuatazo ni faida za matumizi ya mbegu hizi.
1.KULAINISHA NGOZI NA KUPUNGUZA DALILI ZA UZEE (SKIN AND AGING)
Tafiti
zinaonesha kwamba ndani ya mbegu hizi kuna kemikali zinazosaidia
kupunguza makali ya radikali huru (free radicals) zinazotengenezwa
mwilini mwetu na kuleta matatizo mbali mbali kwenye ngozi.Kemikali hizi
zinajulikana kama phenolic ant oxidants.Na kulingana na tafiti Mbegu za
chia ndo chakula chenye ant oxidants nyingi kuliko vyakula vingine.
Soma makala ya utafiti huu hapa: UTAFITI KUHUSU MBEGU ZA CHIA
ANTOXIDANTS
zinasaidia kutengeneza seli mpya za ngozi na kuondoa zile zilizokufa
hivyo kuzuia ngozi kuharibika na kuwa na makunyanzi,Pia kutumia mbegu
hizi inasadia kuepusha seli za ngozi kufa kabla ya muda wake kutokana na
magonjwa.
2.MFUMO WA KUMENG'ENYA CHAKULA (Digestive system)
Mbegu
za chia zina kiwango kikubwa cha Fibers. Kwa kijiko kimoja unapata
11gram za fibers.Kama tunavyojua fibers zinasaidia sana katika
kumeng'enya chakula.
Pia
Taasis ya Ugonjwa wa kisukari nchini marekani (AMERICAN DIABETIC
ASSOSIATION), Na shirika la afya nchini Uingereza (NATIONAL HEALTH
INSTITUTE) wanasema kuwa mbegu za chia zinasaidia kubalance kiwango cha
sukari mwilini hivyo zina faida kwa wagonjwa wa kisukari.Kutokana na
kiwango kikubwa cha fibers ambazo zinasaidia kongosho kuzalisha Insulin
ya kutosha.
Mbegu hizi zina LINELONIC ACID ambayo inausaidia mwili kufyonza VITAMIN A,B,D na E kutoka kwenye vyakula.
Fibers
pia zinasaidia kuimarisha kuta za utumbo Hivyo kusaidia kuondoa tatizo
la kukosa choo au kupata choo kigumu sana (Constipation).
Mbegu
hizi zinasaidia kupunguza uzito kwa watu wenye uzito uliopita kiasi
kwani tafiti zinaonesha kwamba mbegu hizi ziwapo tumboni husharabu maji
na kuvimba hvyo kumfanya mtu ajisikie ameshiba ndo maana tafiti zinasema
mbegu za chia ni nzuri kuondoa njaa ( hunger suppresser) hivyo nzuri
kwa watu walio katika program ya kupunguza uzito ( Diet)
Soma makala ya utafiti hapa : MBEGU ZA CHIA NA KUPUNGUZA UZITO
Pia
mbegu hizi zinapovunjwavunjwa hutengeneza kitu kama mafuta (gel)
kinachosaidia kukua kwa wadudu wanaosaidia kumeng'enya chakula waliopo
tumboni (prebiotic)
3.AFYA YA MOYO
Mbegu
za chia zinasaidia mwili kubalance kiwango cha Lehemu (cholesterol) na
kupunguza hatari ya mtu kupata tatizo la mishipa ya damu kujaa
mafuta(Atherosclerosis) na kupelekea tatizo la shinikizo la damu kuwa
juu, Hivyo mbegu hizi ni muhimu katika kuimarisha afya ya Moyo na
kuondoa hatari ya kupata Tatizo la shinikizo la damu kuwa juu.
Hii ni sehemu ya majibu ya utafiti kuhusu Mbegu za Chia na matatizo ya moyo:
The available human and non-human studies show possible effectiveness for allergies, angina, athletic performance enhancement, cancer, coronary heart disease (CHD), heart attack, hormonal/endocrine disorders, hyperlipidemia, hypertension, stroke, and vasodilatation. Some evidence also suggests possible anticoagulant, antioxidant, and antiviral effects of Salvia hispanica.
4.AFYA YA UBONGO
Chia
seeds zina kiwango kikubwa cha Omega -3 na Omega- 6 Fatty acids ambazo
ni muhimu sana katika kusaidia ubongo kutengeneza seli zake. Virutubisho
hivi ni muhimu sana kwa watoto.chia ni mmea pekee wenye virutubisho
hivi.
5.KUTIBU NA KUKINGA KUPATA UGONJWA WA KISUKARI
Watafiti kutoka chuo -University of Litoral,Argentina
katika utafiti wao waliona kuwa Mbegu hizi zina Alpha Linolenic acid na
Fibers nyingi,vitu hivi vinasaidia kupunguza mafuta kwenye damu(excessive
fat in the blood) na kuzuia tatizo la mwili kushindwa kutumia Hormone
ya insulin ( Insulin resistance) hali inayopelekea kisukari aina ya pili
(type 2 diabetes ) Soma makala ya utafiti huo iliyochapishwa kwenye
jarida la lishe la Uingereza :British Journal of Nutrition
6.KUUPA MWILI NGUVU
Tafiti zilizochapishwa kwenye jarida la Journal
of Strength and Conditioning zinasema kuwa matumizi ya mbegu za chia
huupa nguvu mwili mara mbili ya jinsi vinywaji vya kuongeza nguvu kama
lucozade vinavyoweza kuongeza nguvu ya mwili.
Pia mbegu hizi zinaongeza body metabolism hivyo mwili unatumia mafuta kama chanzo cha nguvu hivyo kusaidia kuondoa kitambi.
7.KUIMARISHA MIFUPA
Kama
tulivyoona mbegu hizi ndani yake kuna kiwango kukubwa cha Madini ya
calcium hivyo husaidia kuimarisha mifupa,pia husaidia kuwakinga watoto
na tatizo la matege.
8.SARATANI YA MATITI NA SHINGO YA KIZAZI
Utafiti
unaonesha kuwa Kemikali ya alpha linolenic acid inasaidia kuzuia
utengenezwaji wa seli za saratani ya Matiti na saratani ya shingo ya
kizazi.Hivyo matumizi ya mbegu hizi husaidia kuwaondoa kina mama katika
hatari ya kupata saratani hizi.
soma utafiti huo hapa: Journal of Molecular Biochemistry
9.AFYA YA MENO
Kutokana
na kuwa na kiwango kikubwa cha madini ya calcium,phosphorous,vitamin A
na zinc mbegu hizi zinasaidia kuimarisha afya ya meno pia.
UJAUZITO
Matumizi
ya mbegu hizi wakati wa ujauzito inasaidia kumpatia mama virutubisho
muhimu vinavyohitajika kipindi cha ujauzito na muhimu katika ukuaji wa
mtoto mfano Omega -3.
JINSI YA KUTUMIA MBEGU HIZI
-Unaweza kuzitafuna mbegu hizi
Unaweza pikia kwenye chakula chako kama mchuzi wa samaki nyama au kuku
- Inafaaa kuchanganya kwenye uji ,maziwa ,juice maziwa mgando, smoothies, fruit salad, vegetable salad etc
- Unaweza nyunyiza juu ya chakula chako wakati wa kula kama wali ndizi supu n.k
- Inafaaa kuchanganya kwenye uji ,maziwa ,juice maziwa mgando, smoothies, fruit salad, vegetable salad etc
- Unaweza nyunyiza juu ya chakula chako wakati wa kula kama wali ndizi supu n.k
Kama unazitumia kwa lengo la kupunguza uzito
Asubuhi
kabla ya kula chochote weka vijiko viwili vya chakula kwenye kikombe
weka maji ya moto ukipenda kamulia limao. Kunywa mchanganyiko huo.
Itakupa nguvu na kukushibisha kunywa chai yako baada ya nusu saaa au
zaidi.
Pia
kabla ya kula chakula una changanya kijiko kimoja kwenye glass moja ya
maji acha itulie kwa nusu saa ndio unywe. au kama unaweza unatafuna
kijiko kimoja cha mbegu hizi unatulia nusu saa ndio unakula
KWA WATOTO
Unaweza
kumchanganyia mtoto kwenye uji,juice, maziwa nk. pia unaweza kuzisaga
mbegu hizi pamoja na viungo vingine vya unga wa lishe au ulezi.
Mbegu
hizi kwa sasa zinapatikana hapa nchini kwetu.endapo unahitaji mbegu
hizi na hujui wapi pa kuzipata wasiliana na namba hii 0762167811 utaelekezwa wapi unaweza kuzipata.







Naweza kupata wapi chia seed
ReplyDeleteKwangu nauza
DeleteNiko iringa
ReplyDeleteIn shaa Allah
ReplyDeleteAsante Doctor
ReplyDeleteNajaribu sana kupiga hzo namba ulizotuwekea lkn haupatkan mkuu!!
ReplyDeleteTunaomba utuandikie na faida ya tende na asali, maana naskia n vitu vinavyocfiwa sana ila sijui kiundan faida zake
ReplyDeleteThanks Dr.Joh.nimeelewa vzr matumizi na faida ya mbegu za chia.lkn je inatakiwa kuzitumia kwa muda gani?ili kuepuka overdosing?
ReplyDeleteAsante kwa Elimu nzuri
ReplyDeleteAsante kwa Elimu hii uliyotupatia tunashukuru sana doct
ReplyDeleteNauza CHIASEED kwa bei rafk kabisa nafanya free delivery DAR ES SALAAM tsh 6000/= gram 500 nichek 0714785775
ReplyDeleteNaweza kuchanganya na maji ya baridi nikatumia kwamuda wa mchana
ReplyDeleteNauza chia kwa mawasiliano 0752301758/0783702570
ReplyDelete