Wakati wa ujauzito wanawake wengi hukosa
hamu ya tendo la ndoa hivyo mwanaume unahitaji kuwa na mawasiliano mazuri ili
mambo yaende vizuri.
JE MWANAMKE MWENYE MIMBA ANAWEZA KUENDELEA
KUFANYA TENDO LA NDOA?
Hakuna ushahidi wa kisayansi unaothibitisha
kwamba tendo la ndoa kwa mwanamke mwenye mimba ya hatua yoyote ya ujauzito
inaweza kumuathiri mwanamke mwenyewe au mtoto tumboni (fetus)
Hivyo tendo la ndoa ni salama kabisa muda
wote wa ujauzito.
JE NI WAKATI GANI MAMA MJAMZITO HARUHUSIWI
KUFANYA TENDO LA NDOA?
Ni pale tu mwanamke anapojisikia kuwa na
bleeding au maumivu yoyote au leakage ya majimaji yajulikanayo kitaalamu
amniotic fluid
Na kama mmoja ya wanandoa ana magonjwa ya
zinaa (STD) haruhusiwi tendo la ndoa hadi daktari athibitishe kwamba amepona
ama sivyo anaweza kusababisha mtoto tumboni aambukizwe.
Pia kama una historia ya tatizo la cervix
Kumbuka!
Pia ifahamike kwamba si wanawake wote
wakiwa na mimba hupenda tendo la ndoa wengine huwa hawapendi kabisa.
Utafiti unaonesha pia kwamba mwanamke
mwenye mimba hukosa hamu ya tendo la ndoa miezi mitatu (3) ya kwanza, then
hupenda sana tendo la ndoa miezi mitatu inayofuata na Pia miezi mitatu ya
mwisho hukosa tena hamu ya tendo la ndoa kwa sababu ya saikolojia ya kusubiri
mtoto kuzaliwa.
Ingawa uzoefu unaonesha kwamba mwanamke
mwenye mimba husisimka haraka na kufika kileleni mapema sana kwa sababu damu
huwa nyingi sana kuzunguka uke na hivyo kuwa sensitive zaidi kuliko akiwa hana
mimba
Kitu cha msingi pia ni kuzingatia mikao au
milalo wakati wa tendo la ndoa kwani mwanamke mwenye mimba anahitaji mikao au
milalo ambayo haikandamizi tumbo lake.

No comments
Post a Comment