MALARIA WAKATI WA UJAUZITO.





Malaria ni maambukizi ya seli nyekundu za damu inayosababishwa na parasiti iitwayo Plasmodiumu zinazobebwa na aina fulani ya mbu jike wajulikanao kama Anopheles. Mbu hutoa parasiti za malaria katika damu ya mtu aliyeambukizwa anaponyonya damu 'chakula', na kisha kupitisha parasiti anapomwuma mtu mwingine, Parasiti hukua na kukomaa katika seli nyekundu za damu na mamilioni ya parasiti hukusanyika katika kondo(placenta) ya mjamzito.

Malaria inaweza kuwa kali zaidi kwa kina mama walio na magonjwa mengine. Malaria ni hatari zaidi kwa wajawazito kuliko watu wengine. Mjamzito aliye na malaria yuko katika hali ya kupata anemia (utakavyoona baadaye katika kipindi hiki), kuharibika kwa mimba (kutoka kwa mimba pekee yake kabla ya wiki 24 za ujauzito), kuzaa mapema, kupata mtoto mdogo zaidi, kuzaa mtoto aliyekufa (mtoto kuzaliwa akiwa amekufa baada ya wiki 24 za ujauzito) au kufa yeye mwenyewe (kifo cha mama).

DALILI ZA MALARIA

Dalili za ugonjwa huwa ishara kwa mwathiriwa na anazifahamu na kuwa na uwezo wa kukueleza kuzihusu; wanaweza kukuambia pekee yao, lakini unaweza kuuliza maswali yanayozihusu. Dalili za malaria ni kama vile:

    1). Baridi (kuhisi baridi isiyo ya kawaida) na kutetemeka (vipindi vikali vya kutetemeka kwa dakika kadhaa na hudumu hadi saa hii huwa dalili ya kwanza ya maambukizi
    2) Maumivu ya kichwa na udhaifu mara nyingi huandamana na baridi
    3)Joto jingi mwilini (halijoto ya juu); Joto jingi mwilini mara nyingi hufuatwa na baridi, na joto linaweza kwenda juu sana hivyo mtu anakabiliwa na deliriumu (kutokuwa katika hali sawa kiakili, kuona au kusikia mambo yasiyohalisi)

   4) baadhi ya hali zingine kuhara/kutapika kunaweza pia kushuhudiwa
    5) maumivu ya misuli/viungo.

Vipindi vya joto jingi kwa kawaida hubadilishana na vile vya baridi na joto kwa malengo ambayo yanaweza kuwa kila siku, au baada ya siku 2-3. Dalili hizi zote zinaweza kutokana na kitu kingine chochote, lakini unapaswa kushuku malaria ikiwa yatatokea kwa mtu ambaye ameumwa na mbu katika eneo ambalo malaria hutokea kila mara.

Ishara za ugonjwa ni ishara kuwa mhudumu wa afya pekee ndiye atakayejua, au kutambua kwa kufanya uchunguzi. Kwa mfano, ukishuku ni malaria, unapaswa kupima halijoto na kipimajoto ukiwa nacho, au kwa kulinganisha hali yako ya joto na ya mama. Mtu akiwa na malaria, joto mwili linaweza kwenda juu hadi sentigredi 39-40 au hata zaidi.

    Ni ipi kiwango cha joto la mwili la kawaida na ishara ya joto jingi mwilini ni ipi?

    Joto la mwili kwa kawaida ni sentigredi 35 hadi 37; ishara ya joto mwilini litakuwa sentigredi 38 au zaidi.

JINSI YA KUBAINI UGONJWA WA MALARIA

Kuna njia mbili kuu za kutambua malaria kwa kutumia uchunguzi wa damu. Njia rahisi ni kufanya uchunguzi wa haraka wa malaria ambao hutambua protini zinazotolewa na parasiti katika damu ya mgonjwa. Vifaa vya kuchunguza vinaweza kuwa aina ya vijiti vya kutumbukiza, plastiki, au kadi, ambazo hubadilisha rangi zinapopata tone la damu kutoka kwa mtu aliyeambukizwa - kwa kawaida huchukuliwa kutoka kwa kidole na shindano safi. Hata hivyo, vifaa vya kuchunguzia lazima vihifadhiwe kwa makini na kutunzwa kutokana na unyevu na joto jingi. Mafunzo kwa wahudumu wa afya yanahitajika kabla ya utambuzi sahihi wa ishara za malaria kwa malengo ya uchunguzi.

Njia nyingine ya kutambua malaria, ambayo inahitaji utaalamu wa mafunzo na vifaa, ni kutokana na uchunguzi wa damu kwa hadubini kwenye kioo, ambacho kimewekwa rangi ilikuonyesha parasiti. Vifaa vya kuchunguzia damu kwa hadubini kwa kawaida havipatikani katika Kituo cha Afya cha ngazi ya chini. Ikiwa umefunzwa kufanya uchunguzi wa malaria wa haraka na unaweza kutumia vifaa vya kufanyia uchunguzi, unapaswa kutoa utambuzi wa malaria kutokana na malengo ya uchunguzi huu. Ikiwa huwezi kutumia vifaa vya kuchunguza malaria kwa haraka, tekeleza utambuzi wako kwa msingi wa dalili (kwa mfano, maumivu ya kichwa, joto jingi mwilini, baridi, maumivu katika misuli /viungo), na joto jingi mwilini iliyopimwa na kipimajoto.

MATIBABU YA MALARIA WAKATI WA UJAUZITO.

Ni muhimu kwa wajawazito kuepukana na malaria - au kutibiwa haraka wakiwa wagonjwa. Ikiwa mama ana dalili za malaria, anapaswa kutibiwa mara moja. Dawa inayotumika mara nyingi huitwa Sulfadoxine/pyrimethamine (SP) ambayo mama mjamzito huanzishiwa pindi anapoenda kliniki kwa ajiri ya kujikinga ma vijidudu vya malaria lakini pia dawa nyingine inayotumika sana katika kutibu malaria ni Artemether Lumifantrine (ALU) (Inauzwa kama Coartem). Uharibu ukuaji wa parasiti katika seli nyekundu za damu za mtu.

Coartem inaweza kutumika kutibu malaria katika awamu ya pili na ya tatu ya ujauzito. Awamu ya pili ni wiki 13-27 tangu wakati wa mwisho wa mama kupata hedhi ya kawaida, na awamu ya tatu ni kutoka wiki 28 hadi wakati wa kuzaa, karibu wiki 40. Malengo ya uchunguzi yakionyesha kuwepo kwa malaria, au ukishuku kuwepo kwa malaria sana kulingana na ishara na dalili, na mama akiwa katika awamu ya pili ama ya tatu.

 Kutibu kwa kutumia Coartem katika awamu ya pili au ya tatu ya ujauzito

    >Tembe 4 za Coartem mara mbili kwa siku (baada ya masaa 12) kwa siku 3 (jumla ya tembe 24). Mshauri ameze na chakula, maziwa, supu au uji wa shayiri. Anaweza kuzivunja na kuzichanganya kwa kijiko cha chakula kama hii itakuwa rahisi kwake kumeza dawa. Mchoro 18.3 inaonyesha jinsi ya kueleza kina mama idadi ya tembe za kumeza.
    >Unaweza pia kumpatia tembe za paracetamol (miligramu 500-1000) kila baada ya saa 4-6 ili kupunguza joto jingi mwilini.
    >Kupangusa mwili wake kwa kitambaa kilichoingizwa ndani ya maji baridi pia husaidia akiwa na joto jingi.
    >Mshauri mama anywe maji mengi ili awe na maji ya kutosha mwilini. Anapaswa kunywa angalau kikombe1kubwa cha maji kila saa.

NOTE: Wajawazito wanaoshukiwa kuwa na malaria katika awamu ya kwanza ya ujauzito, wanaoweza kusafiri, wanapaswa kupelekwa kwenye kituo cha afya kilichoko karibu kwa matibabu maalum.

Mama akiwa katika awamu ya kwanza ya ujauzito (yaani, hadi wiki 12 tangu wakati wa Mwisho wa mama Kupata Hedhi yake ya Kawaida), lakini anaugua sana kusafiri hadi kituo cha afya, mpe matibabu yaliyo ainishwa hapo juu ila zingatia kufika kituo cha afya. Hatari kwa maisha yake na ya fetasi kutokana na malaria, ni kubwa kuliko hatari ya kutumia dawa mapema wakati wa ujauzito.

Jumla ya vifo vinavyotokana na malaria na magonjwa ya malaria zimepungua katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na jitihada kubwa za kuzuia malaria na matibabu ya haraka inapotokea. Mpango huu ni muhimu sana kwa kupunguza malaria hata zaidi, ikiwa ni pamoja na utambuzi na matibabu ya mapema kwa wajawazito wanaokuja kwenu kwa huduma ya ujauzito.

JINSI YA KUJIKINGA NA MALARIA

Ili kukinga malaria, lazima ufanye lolote uwezalo ili usiumwe na mbu. Unapaswa kushauri kila mtu katika jamii wajitokeze pamoja ili:

   1) Kuondoa maji taka yanayoleta mbu; ondoa maji ya mvua kwenye choo; funika au ondoa makopo ya bati na sufuria zinazokusanya maji karibu na nyumba.
   2) Usikae usiku katika maeneo yenye maji ambapo mbu huzalia.
   3) Tumia vyandarua vilivyotiwa dawa ya kuua wadudu, kemikali inayoua mbu. Vyandarua hivi vinalinda watu ambao hulala ndani yao kutokana na mbu, na wao pia hupunguza hatari kwa wale wengine wanaolala katika chumba kimoja nao kwa sababu dawa hii hufukuza mbu wasiingie ndani ya nyumba.

Kukinga malaria inapaswa kuwa wajibu wa mtu binafsi na jamii. Panga kufanya kampeni ya afya kwa lengo la kuhamasisha wana nchi namna ya kukinga malaria, kwa kutumia mbinu za kukuza afya. Hakikisha kwamba wajawazito unao wahudumia wanajua kwamba, watoto wao ambao hawajazaliwa na walio chini ya miaka 5 wote wako katika hatari ya malaria.

AHSANTENI WOTE.

No comments