Usafi na Utunzaji wa Meno ya Watoto

Utunzaji wa meno ya watoto unahitaji uangalizi mkubwa kama ilivyo kwa watu wazima, na upuuzaji wa suala hilo unaweza kuwa na madhara ya muda mrefu maishani. Hii ndio maana madaktari wa meno wanashauri kuwa, ni vyema meno ya watoto yakaanza kusafishwa tangu pale linapochomoza au kuota jino la awali kinywani na ikiwezekana hata kabla ya hapo.

Baadhi ya wataalamu wanashauri wazazi kutumia kitambaa na maji safi kusafishia meno ya mtoto, huku akiwa ameketi katika hali ya utulivu. Itafahamika kuwa bacteria au vijidudu maradhi huishi kwenye sehemu ile ya jino iliyofunikwa na utando wa vyakula uliong'ang'ania kwenye jino.
 Bacteria hao hukutana na chakula na kusababisha asidi na hatimaye hutengeneza tundu au mmomonyoko katika meno. Utando huo unapaswa kuondolewa kila siku wakati unapopiga mswaki ili kuhakikisha kuwa meno na fizi zako ni safi na salama.

Wazazi wanapaswa kuzingatia usafi wao wa kinywa pamoja na wa watoto wao. Vijidudu hivyo maradhi vinapatikana ndani ya mate na kwa hivyo ni rahisi kuenezwa kutoka kwa mzazi hadi kwa moto wakati wa kubusiana au kushumiana na kupitia uchangiaji wa vyombo vya chakula. Wazazi au walezi wanapaswa kubeba jukumu la kusimamia afya ya kinywa ya watoto wao hadi hapo watakapofikia umri wa kati ya mia minane au tisa.

Kwani wataalamu wanasema kuwa katika kipindi hicho, watoto huwa hawana uwezo wa kujisimamia katika kuboresha usafi wa meno unaotakikana. Mtoto anaweza kuanza kusafisha meno yake kwa kutumia mswaki vile inavyotakikana chini ya usimamizi wa wazazi au walezi akiwa na umri wa miaka saba.

Usafi wa kinywa na meno unapaswa kuanzishwa hata kabla ya mtoto hajaanza kuota meno. Fizi za watoto wachanga na wale wa chekechekea zinaweza kusafishwa kwa kufutwa kwa utaratibu kwa kutumia shashi au gauze, au hata kitambaa kisafi chenye unyevunyevu. Kitendo hicho huchangamsha pia fizi za mtoto na kusaidia kupunguza baadhi ya maumivu ambayo huwapata watoto wakianza kuota meno. Madaktari wa meno wanasema kuwa, mara meno ya mtoto yanapochomoza , yanapaswa kusafishwa kwa mpangilio angalau mara mbili kwa siku, baada ya kifungua kinywa na kabla ya kulala, yaani usiku, bila ya kusahau ulimi.

Imeelezwa kuwa kwa watoto wadogo yaani wale wa chekechea, wazazi wanashauriwa kutumia kiwango kidogo cha dawa ya meno yaani dawa hiyo iwekwe kwenye shashi au gauze na wasafishe meno ya watoto wao kwa utaratibu. Na ikiwa meno yote ya mbele ya mtoto wako yameota, unashauriwa kutumia mswaki mdogo wa watoto. Njia nyepesi ya kumsafisha mtoto ni kuhakikisha kuwa kichwa chake kimejiegemeza kwenye mapaja yako, ili uweze kuona vyema ndani ya kinywa chake na kuyasafisha kama inavyotakikana, huku mtoto akiwa katika hali ya utulivu. Na iwapo mtoto atakuwa mkubwa kuanzia miaka saba anaweza kusimama mkabala na mzazi wake huku ukikiinua kichwa chake ilikuweza kufikia na kuona vizuri meno yote.

 Mara nyingine wazazi wamekuwa akishuhudia watoto wao wakitokwa na damu kwenye fizi wakati wakipigwa mswaki. Jambo hili lisiwazuia wazazi kuwasafisha meno watoto wao. Kuvuja damu fizi ni ishara ya kuathiriwa na maradhi. Kwa hiyo uvujaji huo wa damu hutatokomea iwapo utando unaong'ang'ania kwenye meno na bacteria au vijidudu maradhi vitaondolewa.

Kwa kuzingatia kuzagaa aina mbalimbali za dawa za kusafisha meno(au tooth paste) katika maduka mbalimbali hivi sasa, wazazi wanakabiliwa na halingumu katika kuchagua dawa ipi ni bora kwa usafi na utunzaji wa meno ya watoto. Lililo na umuhimu hapa ni kufahamu kiasi kinachotakikana kutumia katika mswaki wa mtoto wako na si aina ya dawa. Kiasi kidogo tu cha dawa ya meno kinatakikana kwa mtoto wako na si kurundika lundo la dawa, hiyo haina faada yoyote ghairi ya kumletea madhara.
Dawa ya meno haipaswi kumezwa. Hatua ya kumeza au kulal kiasi kikubwa cha dawa ya kusafishia meno inazidisha hatari ya kuoza meno ya muda ya watoto yaani(permanent teeth, khususan kwa watoto walio na umri chini ya miaka mitano. Kwa sababu hiyo wataalamu wa meno hawashauri kutumia dawa za kusukutulia kinywa yenye kampaundi ya fluoride kwa watoto chini ya miaka sita, kwa sababu hawawezi kujizuia kumeza na hivyo huwa na uwezekano mkubwa wa kukumbwa na maradhi ya fluorosis.

Je mnafahamu kuwa chakula kina athari kubwa katika afya ya kinywa na meno ya mtoto wako?Uchaguzi wa vyakula na mipangilio ya ulaji inayoasisiwa tangu kipindi cha utotoni unaweza kuwa na taathira kwa afya ya uhai wa maisha yako yote. Mlo kamiliunaojumuisha vyakula vya aina tatu kwa siku(Yaani protini,vitaminina wanga ) unapaswa kushajiishwa. Hatua ya kujumuisha mada za protini katika milo hiyo husaidia watoto kutohisi njaa haraka, na hivyo kumfanya mtoto kukosa hamu ya kukimbilia kula vyakula visivyo na manufaa kama vile vyenye sukari nyingi.  miendo bora ya ulaji chakula pamoja na usafi wa kinywa unaotakikana si tu kuwa humuepusha mtoto kuoza na kuharibika kwa meno yake, bali pia humfanya mtoto kimwili kuwa katika afya njema.

No comments