Kwa kawaida
kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu mbalimbali vyenye kuleta athari kwa
afya kama vile vimelea vya magonjwa kama vile bakteria na virusi, lakini wakati
mwingine pia na vitu ambavyo havina madhara yoyote kwa mwili, ambavyo huitwa allergens (mzio).
aleji au
mzio (allergy) ni matokeo ya kinga ya mwili inapofanya kazi ya ziada ya
kupambana na kitu chochote ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa mwili
pale inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili.
Kinga ya mwili
inapoamua kufanya kazi ya ziada husababisha mtu kuwa na dalili za aleji au mzio
katika mwili wake kwa kuona dalili mbalimbali
Vitu vinavyosababisha mzio
baadhi ya
vitu vinavyosababisha mzio ni pamoja na vumbi, baadhi ya dawa zenye madini ya
sulfer, vyakula, kung’atwa na wadudu kama vile nyuki na baadhi ya uyoga.
wapo pia
watu ambao wanapatwa na mafua karibu kila siku na wengine kushindwa kuvaa aina
fulani ya nguo na vitu kama saa,hereni na cheni, kwani mara nyingi husababisha
kuwashwa na kuvimba mara wavivaapo.
watu wenye
mzio huwa na hisia zisizo za kawaida za mwili dhidi ya vitu vinavyowaathiri na
pindi mwili unapokumbana na vitu vinavyosababisha mzio, mfumo wa kinga wa mwili
huzalisha kemikali mbalimbali, mfano histamine ambazo hupambana na mzio.
Mara
nyingine watu hupata ugonjwa wa mzio pindi wanapokutana na aina fulani ya
mazingira kama yenye vumbi, baridi ya wengine hupatwa na mzio wanapopigwa na
jua kali au msuguano wa ngozi unaweza kuwasababishia dalili fulani za mzio.
Dalili zake
mara nyingi dalili
hutegemeana na mgonjwa ana aina gani ya mzio.
Kama mtu
atakuwa na mzio katika mfumo wa hewa, huweza kupata matatizo ya kupumua
anapokutana na mazingira yenye vumbi, hali inayomsababishia kupiga chafya mara
kadhaa, kutokwa na makamasi, kuziba pua, muwasho kwenye pua na koo au kupumua
kwa kutoa sauti kama filimbi, kuumwa na kichwa mara kwa mara, kizunguzungu,
pumu, kuhisi joto katika mwili na mfadhaiko.
Endapo macho
yataguswa, mhusika huhisi hali ya macho kuchoma, kutiririkwa na machozi na
muwasho kwenye macho na pindi anapojikuna, macho huvimba na kuwa mekundu.
Iwapo mtu
atakula kitu ambacho ana aleji au atakunywa dawa zenye sulfer na zina mzuru
kila azitumiapo, anaweza kuwa na dalili kama ya kuharisha, kichefuchefu,
kutapika, kusokotwa au kuumwa na tumbo na hata hali mbaya ya kutishia maisha.
vitu
vinavyosababisha aleji vinapogusa ngozi ya binadamu, vinaweza kusababisha ngozi
kuwa na mabaka, kubabuka, kuvimba, muwasho, kutoa vipele, malengelenge,
michubuko na ngozi kuwa nyekundu.
Zipo aleji zinazohusisha
mwili mzima zinaweza kuwa na mkusanyiko wa dalili zote alizozitaja na wakati
mwingine mtu anaweza kuwa na aina fulani ya nguo, hivyo vyema kuziepuka ili
kupunguza tatizo hili.
Maambukizi
Kwa kawaida
ugonjwa wa mzio huwa ni wa kuzaliwa nao na hauambukizi ikiwa mtu katika familia
ana ugonjwa huo, hawezi kumuambukiza mtu mwingine.
Jinsi ya kufanya vipimo
mara nyingi
mgonjwa wa mzio hupimwa kwa kutumia damu kwa sababu katika damu inaweza kutoa
majibu ya mgonjwa juu ya mzio alionao na hii ni baada ya mgonjwa kuelezea vitu
gani vinavyomsababishia matatizo mara avitumiapo.
Na hii ni
kwa sababu kuna baadhi ya mambo yanayoweza kumsababishia mtu dalili
zinazofanana na za mtu aliye na aleji ya kitu fulani
Kwa mfano,
matumizi ya aina fulani ya dawa yanaweza kumsababishia mtu mikwaruzo au
michubuko katika ngozi inayofanana na aleji nyingine, au mtu anaweza kuwa na
mafua au kikohozi kwa sababu ya maambukizi ya bakteria au virusi na si kwa
sababu ya aleji.
Anasema mara
nyingine wanapopima damu huangalia ongezeko la immunoglobin E ambayo huashiria
uwapo wa vitu vinavyosababisha aleji na kipimo cha damu chenye kuonesha
ongezeko la eosinophil iwapo kuna aleji, ambayo ni sehemu ya chembe nyeupe
za damu.
Matibabu
Shambulio
kali la aleji linaweza kusababisha mhusika kulazwa hospitali na
lisipodhibitiwa, kifo kinaweza kutokea kutokana na kupata shida katika upumuaji
wake, lakini hii hutokea mara chache kwa wagonjwa wenye mzio katika chakula na
mfumo wa hewa.
Anasema tiba
kubwa ni kupunguza uwezekano wa kupata aleji kwa kutambua na kuepuka kitu au
vitu vinavyokusababishia hali hiyo.
Kama ni
chakula au dawa au kemikali, mgonjwa anatakiwa kuepuka kabisa matumizi yake, na
kama ni vumbi ajitahidi kukaa nalo mbali
zipo pia
aina mbalimbali za dawa zinazotumika kutibu na kuzuia aleji, kulingana na jinsi
daktari atakavyoona inafaa kwa kuzingatia ukali wa tatizo, dalili zake
azipatazo mgonjwa, umri wa mgonjwa pamoja na hali yake ya kiafya kwa ujumla.
Anasema pia
wagonjwa hawa hupewa dawa maalum kwa ajili ya kutuliza mcharuko mwilini ambazo
huwa katika miundo mbalimbali zikiwamo za kupaka, matone, kuvuta, sindano au
vidonge.
Kwa wale
wenye mafua na kuziba kwa pua, hushauriwa kutumia dawa zinazosaidia kufungua
pua, hata hivyo, dawa hizi hazina budi kutumiwa kwa uangalifu hasa kwa watu
wenye magonjwa ya shinikizo la damu au moyo.
Anasema
wagonjwa hawa hupewa dawa pia kwa ajili ya kuzuia vitu vinavyosababisha aleji.
Aina nyingi
za aleji hutibika kwa urahisi kwa kutumia dawa. Wapo baadhi ya watu
hususan watoto wanaoweza kujenga hali ya aleji dhidi ya aina fulani za vyakula,
hali wanayoweza kuendelea nayo hadi ukubwani na kwa kawaida, kitu kikimletea
mtu aleji utotoni, huendelea kumuathiri daima
Madhara yatokanayo na mzio
madhara ya
mzio ni pamoja na kupata shambulio kali ambalo linaweza kusababisha kifo kama
matibabu hayatafanywa haraka.
Kuna baadhi
ya watu ambao wakila baadhi ya vyakula huvimba mwili na kushindwa kupumua mpaka
kuhitaji kulazwa hospitali na kusaidiwa kupumua kwa mashine.
Madhara
mengine ni pamoja na shida ya kuvuta pumzi au kushuka kwa shinikizo la damu
(kupata shock).
Namna ya kujikinga na aleji
kuna baadhi
ya wagonjwa hupata madhara makubwa ya kuungua nje na ndani pindi wanapotumia
dawa ambazo zina sulfer na huwasababishia mzio ambao usipotibiwa kwa haraka,
kifo kinaweza kutokea.
“Steven
Johanson’s syndrome ni mzio hatari na wa kipeke kuliko aina zote na mgonjwa
anapopata aina hii ya mzio na ngozi yake huungua nje na ndani na endapo
akichelewa kupewa matibabu huweza kupoteza maisha
Jinsi mzio unavyonyima uhuru wa kufanya kazi
Evelyn Menas
mkazi wa Mtoni Kijichi, anasema yeye mara nyingi hupata tatizo la mzio akikaa
au kupita eneo lenye vumbi au kutokwa na jasho mwilini, mambo yanayomnyima
uhuru wa kufanya kazi katika baadhi ya mazingira.
“Nikitokwa
jasho mwili huwasha, najikuna, kukosa uhuru na mara nyingine ninapokuwa sehemu
yenye hewa iliyo na asili ya vumbi, napiga chafya mfululizo, kuwashwa uso na
macho yanavimba na huwa nashindwa kupumua vizuri kwa sababu pua zinaziba,”
anasema Evelyn.
Anasema
anajitahidi kuhakikisha chumba anacholala kinakuwa safi muda wote, lakini hali
inakuwa ngumu akiwa katika vyombo vya usafiri kama daladala iliyojaza abiria
kupita kiasi, kupita sehemu yenye harufu mbaya, au kutimuliwa vumbi barabarani.
Ushauri
ni vizuri
watu wakazingatia na kufanya utafiti ili kuweza kugundua ni kitu gani
kinawasababishia mzio au kufika katika kituo cha afya kinachotoa huduma ya
vipimo waweze kufanyiwa vipimo na kupata ushauri wa kitaalamu.
Na endapo
mtu atatumia dawa zenye madini ya sulfer zikamletea madhara, anatakiwa awahi
kumuona daktari ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.
Ufahamu undani wa Mzio au Aleji Utokanao na Dawa.
Mzio au aleji ni matokeo ya mpambano uliopitiliza kati
ya kinga ya mwili na kitu chochote ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa
mwili, inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kugusa sehemu fulani ya
mwili.
Katika mjumuisho wa haya yote hali inaelezeka kuwa
mzio ni hali inayotokea wakati seli za mwili wa binadamu zinapokataa kitu ambacho
kwa mtu wa kawaida hakina madhara. Mzio hujitokeza kwa alama au dalili
mbalimbali na huleta matokeo yenye ishara nyingi mwilini.
Kuna aina mbili kuu za mizio zinazosababishwa na kitu
ambacho kiko nje ya mwili na husababishwa na mazingira ya nje ya mwili. Aina
nyingine kuu ya mzio ni ile ambayo iko ndani ya mwili wako ambayo inaweza
kuletwa na kinasaba cha kurithi au na kitu kilichoko ndani ya mwili.
Mzio wa ngozi au aleji inayojitokeza kwenye ngozi ni
tatizo linaloweza kukupata kutokana na mwili kutopenda kitu Fulani kutokana na
sababu kadhaa ikiwemo hewa na hata chakula tunachokula.
Kuna vitu ambavyo huibua mzio kama vumbi katika
nyumba, mavi ya panya, manyoya ya wanyama na hewa yenye aina ya spiriti. Mzio
unaweza kukufanya uwe na ukurutu, mafua, pumu na hata kuvimba kwa mwili ambapo
pia wapo watu ambao hupata tatizo la ngozi, kuwashwa na hata kuvimba.
Katika dunia ambayo inatamba na teknolojia, tatizo la
mzio ni kubwa na hasa kutokana na kemikali zinazotumika katika vyakula na hata
urembo vinapotibua kemikali zinazotengeneza aleji katika mwili.
Wakati kitu chochote kinaweza kuwa alejeni lakini kuna
vitu vingine ambavyo husababisha mzio zaidi kupita kiwango cha kawaidacha hali
ya hewa.
Alejeni zinaweza kuwa vumbi na mazingira
yaliyochafuliwa kwa unga wa mimea na maua, vipodozi na marashi ya kujipaka au
ya kupuliza, vyakula mbalimbali kama mayai, karanga, kemikali zinazotumika
kuhifadhia vyakula na vinywaji ambazo mtu huzila kwenye chakula au kuzinywa
kwenye vinywaji hivyo.
Mzio unaweza kusababishwa na mabaki au uchafu wa
kemikali kutoka viwandani, moshi wa magari machakavu, mwanga wa jua, nyuzi za
nguo zinazotengenezwa viwandani, baadhi ya dawa, manyoya, sufi ya ngozi za
wanyama, wadudu mbalimbali kama mchwa na mende, manyoya ya paka na mbwa na hata
harufu inayotokana na rangi mbalimbali.
Katika hali ya ufahamu zaidi unatakiwa kufahamu kuwa
hali ya Mzio unaosababishwa na dawa au drug allergy ni hali isiyo ya kawaida
inayooneshwa na mfumo wa kulinda mwili kutokana na dawa.
Aleji ya dawa si sawa na athari ya dawa, inayoweza kujitokeza baada ya kula dawa ya aina fulani, ambayo kwa kawaida huambatanishwa na maelezo ya dawa. Mzio unaosababishwa na dawa pia ni tofauti na sumu ya dawa ambayo hutokea pale dawa inapotumiwa kwa kiasi kikubwa ambapo dawa hizo zimetajwa kuwa ni aina za antibiotiki.
Aleji ya dawa si sawa na athari ya dawa, inayoweza kujitokeza baada ya kula dawa ya aina fulani, ambayo kwa kawaida huambatanishwa na maelezo ya dawa. Mzio unaosababishwa na dawa pia ni tofauti na sumu ya dawa ambayo hutokea pale dawa inapotumiwa kwa kiasi kikubwa ambapo dawa hizo zimetajwa kuwa ni aina za antibiotiki.
Uwezekano wa aleji kujitokeza ni mkubwa zaidi pale
dawa inapotumiwa mara nyingi, inapopakwa juu ya ngozi au kudungwa mwilini kwa
sindano, kuliko wakati inaponywewa kupitia mdomo kwa maana na maneno mengine
tunaweza kusema kuwa, mzio wa dawa humaanisha kuwa mwili umekataa dawa fulani
au haupatani nayo.
Dalili za aleji inayosababishwa na dawa kwa kawaida hutokea katika kipindi cha saa moja baada
ya kutumiwa kwa dawa. Mara chache aleji huweza kutokea baada ya masaa, siku au
wiki kadhaa.
Miongoni mwa dalili za mzio wa dawa ni vipele vya
ngozi, muwasho, kuvimba, macho kutoa machozi na ngozi kubadilika rangi. Dalili
nyinginezo za aleji ya dawa ni homa, kuvimba, kubanwa na pumzi, mafua na
kupumua kwa kutoa sauti kama mtu anayepiga filimbi hali inayojulikama kitaalamu
kama wheezing.
Mara chache mzio wa dawa huweza kusababisha madhara
makubwa kwa mtu ambapo mwili huonesha dalili ya jumla inayohatarisha maisha
ijulikanayo kama Anaphylaxis ambayo hukwamisha utendaji wa mfumo wa mwili.
Viashiria vya hali hiyo ni kubwanwa njia ya hewa na
koo, suala linalopelekea kushindwa kupumua. Kichefuchefu au maumivu ya tumbo
yasiyo ya kawaida, kuharisha au kutapika, kizunguzungu au kuhisi kichwa
chepesi, mwili kudhoofika na mapigo ya moyo kwenda mbio. Pia mwenye hali hiyo
presha yake hushuka, huwa na dalili za kifafa na kupoteza fahamu.
Vilevile kuna matatizo ambayo yanaweza kujitokeza
baada ya siku au wiki kadhaa baada ya kutumia dawa, ambayo yanaweza kubakia kwa
muda mrefu hata baada ya kuacha kutumia dawa. Matatizo hayo yametajwa kuwa ni
ugonjwa wa Serum ambao husabisha homa, maumivu ya viungo, vipele, kuvimba na kichefuchefu
pamoja na ukosefu wa damu ambapo chembe nyekundu za damu hupungua na pia
kuvimba figo na kutokewa na vipele vinavyoambatana na matatizo katika seli
nyeupe za damu.
Muhimu kujua ni kwamba utatumia dawa na kwa bahati mbaya zikakuletea aleji
unapaswa kumuona daktari mara moja au kwenda hospitali haraka ili kupata
matibabu na kuondoa aleji na iwapo utapata dalili zinazoashiria
Anaphylaxis kama tulivyoeleza kabla unapaswa kuomba haraka msaada wa kitiba ili
kuokoa maisha.
Cha zaidi unapaswa kuacha kutumia dawa
iliyokusababishia dalili kali za mzio pindi tu unapobaini tatizo hilo baada ya
kubaini tatizo hilo.

Sijaona dawa halisi tafadhari tunaomba usaidizi tatizo linasumbua sana
ReplyDeleteSijaona dawa halisi tafadhari tunaomba usaidizi tatizo linasumbua sana
ReplyDelete