Watoto na
wajawazito ni miongoni mwa makundi katika jamii zetu ambayo yanapewa uangalizi
wa karibu sana. Ili watoto waweze kukua vizuri na pia kwa wamama wajawazito
kuweza kujifungua watoto wenye afya bora, ni vyema pia swala la hewa inayovutwa
na watu hawa ikawa na usalama wa kutosha.
Pamoja na uvutaji
wa sigara na moshi wake kuwa na madhara ya kiafya kwa watu wote, napenda
kuchukua nafasi hii kukushirikisha na uweze kukumbuka au kuyafahamu madhara yanayopatikana
kwa watoto kuvuta hewa iliyo na moshi wa sigara na pia madhara ya uvutaji wa
sigara kwa wamama wajawazito.
Kabla ya
kukufahamisha madhara yanayoletwa na sigara au moshi wake, tuangalie kwanza ni
kemikali gani ambazo zinapatikana katika sigara au moshi wake. Katika moshi wa
sigara baadhi ya kemikali zinazopatikana ni zifuatazo: Nicotine, Carbon
monoxide, Arsenic, Ammonia, Hydrogen Cyanide, Benzene pamoja na Vinyl chloride.
Kwa mama mjamzito
anayevuta sigara au ambaye yupo katika mazingira ya moshi wa sigara (Anavuta
sigara bila kujifahamu au bila lidhaa yake), husababisha madhara yafuatayo kwa
mtoto aliyeko tumboni:
Upungufu wa hewa (
Oxygen) kwa mtoto tumboni, hii husababishwa na kemikali (Carbon monoxide)
ambayo hupunguza na kuzuia damu isibebe oxygen, hivyo mtoto tumboni anakosa
hewa ya kutosha na kumsababishia matatizo katika ukuaji wake wa ubongo, hii pia
hupelekea mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo ya akili.
Mtoto kuzaliwa
akiwa na matatizo au hatari ya kupata magonjwa ya moyo, hii husababishwa na
kemikali (Nicotine) ambayo hupenyeza katika mfuko wa uzazi (Placenta) na
kumfikia mtoto, husababisha mishipa yake ya damu kuwa miembamba zaidi na hivyo
kumfanya apate au awe katika hatari ya kupata magonjwa ya moyo.
Mtoto kuzaliwa
akiwa na uzito mdogo kuliko kawaida (chini ya kilo mbili na nusu), hii
husababishwa na mtoto kukosa hewa ya kutosha pamoja na sumu tofauti tofauti
zilizoko katika moshi wa sigara kumuathiri ukuaji wake.
Pia husababisha
mama mjamzito kupata matatizo mbalimbali yanayohusiana na ujauzito, (Pregnancy
complications).
Kuwa jirani na mtu
anayevuta sigara, inamaanisha wewe unaivuta ile sigara bila kujifahamu
(Secondhand smoke), fikiria mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja yupo mazingira ya
moshi wa sigara, labda ni baba, mama au mtu yeyote anavuta sigara karibu na
mtoto mdogo……kwa watoto wadogo, moshi wa sigara unayo madhara yafuatayo:
Watoto wadogo,
viungo vya miili yako ni vichanga bado, mfano mapafu au mfumo wa upumuaji,
moyo, ini na viungo vingine, moshi wa sigara humfanya mtoto awe katika hatari
ya kupata magonjwa ya mfumo wa upumuaji kama vile pumu, neumonia (pneumonia),
pia kwa muda mrefu huongeza hatari ya mtoto kupata magonjwa ya kansa, magonjwa
ya moyo, magonjwa ya masikio pamoja na macho.
Inawezekana kuvuta
sigara ni jambo la lazima kwako, basi usivute sigara karibu na mama mjamzito,
watoto wadogo, mama mjamzito epuka sigara au moshi wake ili kumlinda mtoto
aliyeko tumboni, pia ni ustaarabu mzuri kutovuta sigara maeneo yenye mkusanyiko
wa watu (Public Areas).

No comments
Post a Comment