Typhoid au kwa kiwahili Homa ya matumbo ni
ugonjwa unaosababishwa na bakteria anayeitwa Salmonella Typhi. Ugonjwa huu
huambukizwa kwa mtu kula au kunywa chakula au maji yalio na kinyesi cha mu
aliyambukizwa. Bakteria hawa hutoboa na kunyonya chakula kwenye tumbo la
binadamu.
Naandika mada hii ili kushirikishana na
wasomaji wangu na jamii kwa ujumla kutokana na mfanano mkubwa wa dalili za
Typhoid na Malaria. Wengi hutibu malaria kwa kumeza dawa tu ambapo hupelekea
kutokupona kumbe tatizo si malaria bali Typhoid. Na Typhoid ikichelewa kutibiwa
huwa ni tatizo zaidi. Kwa hiyo fuatana nami katika mada hii upate kuujua vizuri
ugonjwa huu wa homa ya matumbo
DALILI ZA TYPHOID
Homa kali
Kutoka kwa majasho mengi
Kuharisha (bila ya kutoa damu)
Mara nyingine, vitone vyekundu huonekana
kwenye mwili.
Kwa kawaida, homa ya matumbo isipotibiwa
hugawanyika katika hatua nne, kila hatua ikichukua takriban wiki moja.
Katika wiki ya kwanza:
Joto la mwili huongezeka
Kichwa huuma
Kukohoa
Damu kutoka kwa pua, ingawa tukio hili huwa
ni nadra kutokea.
Maumivu ya tumbo pia huweza kutokea
Katika wiki ya pili:
Homa huongezeka
Mgonjwa huanza kupagawa, kama mwenda wazimu
Vitone vyekundu huanza kutokea kwenye kifua
Mgonjwa huharisha, takriban mara sita au
nane kwa siku.
Kutapika kwa mgonjwa
Ini la mgonjwa huvimba
Homa ya mgonjwa huongezeka katika wakati wa
alasiri kwenye wiki ya kwanza na ya pili.
Wiki ya tatu:
Matumbo hutoa damu.
Matumbo hutoboka
Wiki ya tatu ikimalizika, homa
huanza`kutilia. Hii huendelea hadi wiki ya nne.
TIBA YA TYPHOID
Mara nyingi haishauriwi kununua dawa kabla
ya kujua ni ugonjwa gani unakusumbua hivyo inashauriwa kwenda hospitali au
maabara kupima ili kujua tatizo linalokusumbua.
Dawa kama ciprofloxacin , chloramphenicol, au Ceftriaxone hutumika kutibu
wagonjwa katika nchi zilizoendelea
KINGA YA HOMA YA MATUMBO
Usafi wa mazingara na wa kibinafsi ni hatua
bora ya kujikinga kutokana na ugonjwa huu.
Homa ya matumbo haiathiri wanyama kwa hivyo
maambukizi ni kutoka kwa binadamu mmoja hadi mwingine.
Homa hii huweza kuenea kwenye mazingara
ambayo kinyesi cha binadamu hutangamana na vyakula vyao. Upishi wa makini na
uoshaji mikono ni kingo bora zaidi kwa kuzuia maradhi haya kuenea.
Chanjo ni za aina mbili: moja inayotiwa kwa
njia ya mdomo iitwayo Ty21a (au Vivotif Berna) na nyingine ya sindano kwa
majina Typhim Viiliyotengenezwa na Sanofi Pasteur au Typherixiliyotengenezwa na
GlaxoSmithKline


No comments