kila mwezi mabadiliko ya homoni huuandaa mfuko wa uzazi ‘uterus’
kutengeneza ukuta mpya ‘endometrium’ kwa ajili ya kujiweka tayari kwa mapokezi
ya mimba inayoweza kutungwa.
Kama yai litaachiliwa na kutorutubishwa na mbegu za mwanamme, basi ukuta wa
mfuko wa uzazi humeguka na kutoka nje ukiwa pamoja na damu kupitia ukeni.
Kitendo hiki cha mzunguko hadi kutoka kwa damu ndicho huitwa hedhi
(menstruation) au mzunguko wa hedhi (menstrual cycle).
mzunguko wa damu umegawanyika katika maeneo makuu mawili
1.
MZUNGUKO WA DAMU UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE)
2.
MZUNGUKO WA DAMU USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE)
Napenda tufahamu kwa kina mizunguko hii
MZUNGUKO WA HEDHI UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hutokwa na ute ute wa Uzazi ambao unavutika na katika mzunguko huu mtu anaweza kupata ujauzito
MZUNGUKO WA HEDHI USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hatoki ute ute wa Uzazi hivyo hawezi kupata ujauzito
~ pamoja na mizunguko hii miwili kutofautiana mwanamke hupata hedhi kama kawaida hata hivyo mwanamke ambaye mzunguko wake wa Hedhi hapati ute ute wa Uzazi hawezi kupata ujauzito kutokana na mabadiliko ya mfumo wa homoni
pia napenda mfaham kuwa ute ute wa Uzazi umegawanyika katika Makundi makuu matatu ambayo ni
MZUNGUKO WA HEDHI UNAOPEVUSHA MAYAI (OVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hutokwa na ute ute wa Uzazi ambao unavutika na katika mzunguko huu mtu anaweza kupata ujauzito
MZUNGUKO WA HEDHI USIOPEVUSHA MAYAI (ANOVULATORY CYCLE) ~katika mzunguko huu mwanamke hatoki ute ute wa Uzazi hivyo hawezi kupata ujauzito
~ pamoja na mizunguko hii miwili kutofautiana mwanamke hupata hedhi kama kawaida hata hivyo mwanamke ambaye mzunguko wake wa Hedhi hapati ute ute wa Uzazi hawezi kupata ujauzito kutokana na mabadiliko ya mfumo wa homoni
pia napenda mfaham kuwa ute ute wa Uzazi umegawanyika katika Makundi makuu matatu ambayo ni
UTE MWEPESI
UTE UNAOVUTIKA
UTE MZITO
Mara nyingi wanawake wasiopevusha mayai hawawezi kupata ujauzito hivyo huwa hawapati ute wa Uzazi na pia wengine hupata ute mzito daima kama uchafu unaotoka ukeni Lakini wenyewe hauna harufu wala muwasho
UTE UNAOVUTIKA
UTE MZITO
Mara nyingi wanawake wasiopevusha mayai hawawezi kupata ujauzito hivyo huwa hawapati ute wa Uzazi na pia wengine hupata ute mzito daima kama uchafu unaotoka ukeni Lakini wenyewe hauna harufu wala muwasho
Mzunguko wa kawaida ni upi?
Mzunguko wa hedhi huanzia siku ya kwanza ya kutoka kwa damu hadi siku ya
kwanza tena ya kutoka damu ya mzunguko unaofuata. Japokuwa mzunguko wa hedhi wa
kawaida ni siku 28, ni jambo la kawaida kuwa na mzunguko wenye siku pungufu au
zaidi ya hizo.
Mzunguko huu huweza kutofautiana kati ya wanawake lakini pia kati ya
mzunguko mmoja na mwingine. Mzunguko wa kawaida huwa na siku 21 hadi siku 35
kwa wanawake wakubwa na siku 21 hadi 45 kwa wasichana wadogo walioanza hedhi.
Kwa miaka michache ya awali baada ya msichana kupata hedhi yake ya kwanza
(kuvunja ungo), kupata mizunguko mirefu huwa ni jambo la kawaida. Mizunguko
huanza kupungua urefu (idadi ya siku) na kuanza kuwa ya kawaida kadri umri
unavyosonga na mara nyingi mzunguko huwa kati ya siku 21 hadi 35.
Msichana huanza kupata hedhi (period) wakati gani?
Kwa kawaida, msichana huanza kupata hedhi ya kwanza (menarche) afikapo umri
wa miaka 11-14. Hata hivyo, hedhi huweza pia kutokea binti angali na miaka 8 na
hali hii huwa ni kawaida pia. Umri wa wastani ni miaka 12 lakini hii
haimaanishi kwamba wasichana wote hupata hedhi ya kwanza katika umri sawa.
Mara nyingi hedhi ya kwanza huanza miaka miwili baada matiti ya binti
kuanza kutokeza. Iwapo binti hajapata hedhi ya kwanza angali na miaka 15 au ni
miaka 2 hadi 3 baada ya kuanza kuota matiti, anapaswa amuone daktari.
Ukomo wa hedhi ni wakati gani?
Mwanamke huanza kupata ukomo wa hedhi (menapause) anapofika umri kati ya
miaka 45-55. Wanawake wengine hupata ukomo wa hedhi angali na umri mdogo zaidi
kwa sababu mbalimbali ikiwemo kufanyiwa upasuaji au baadhi ya matibabu, kuugua
au sababu nyingine.
Katika hali ya kawaida, mwanamake huanza kupata hedhi chache anapofika umri
wa miaka 40 ambapo huanza kupata mizunguko mirefu na inayobadilika mara kwa
mara. Mizunguko huanza kuwa mirefu na baadaye kukoma kabisa.
Hedhi ya kawaida ni ipi?
Wakati wa hedhi, mwanamke hutokwa na mchanganyiko wa damu pamoja na ukuta
wa mfuko wa uzazi uliomeguka kupitia sehemu ya uke. Kiasi cha damu inayotoka
(menstual flow) huweza kutofautiana kati ya mizunguko. Kwa wastani mwanamke
hutokwa na damu ya hedhi kiasi cha ujazo wa mililita 35 (sawa na vijiko viwili
na nusu vya chai).
Hata hivyo, kutokwa na damu inayofikia mililita 10 hadi 80 (kijiko 1 hadi
vijiko 6) bado huchukuliwa kama hali ya kawaida.
Wanawake wengi hupata hedhi inayodumu kwa siku 3-5, lakini hedhi yoyote
inayodumu siku 2-7 huwa ya kawaida. Kabla ya hedhi kuanza, wanawake wengi
hupatwa na dalili mbalimbali.
Dalili zinazowapata zaidi ni pamoja na kutokwa chunusi, matiti kuuma,
kuhisi uchovu, kukasirika haraka na kubadilika kwa ukimwa (mood). Hata hivyo,
kiwango cha dalili hizi hutofautiana kati ya wanawake na wengine huwa na dalili
kali zaidi.
Nini hutokea mwilini wakati wa mzunguko wa hedhi?
Mzunguko wa hedhi huendeshwa na homoni mbalimbali za mwili. Wakati wa
mzunguko wa hedhi, sehemu za kwenye ubongo ziitwazo ‘hypothalamus’ na
‘pituitary gland’ hupeleka taarifa za homoni kwenda kwenye ovari na kurudi
kwenye ubongo. Taarifa hizi huziweka ovari na mfuko wa uzazi tayari kwa ajili
ya kubeba mimba.
Kwanza pituitary gland hutoa homoni iitwayo Follicle Stimulating
Hormone-FSH ambayo huenda kusababisha kukomaa kwa yai ndani ya ovari. Baada ya
hapo homoni ya estrogen hutolewa ambayo huenda kusaidia ujenzi wa ukuta wa
mfuko wa uzazi kwa ajili ya maandalizi ya mimba inayoweza kutokea (kwenye ukuta
huu ndipo mimba hujishika, kupata virutubisho na kukua).
Wakati kiwango cha estrogen kimepanda mwilini, hali hii husababisha
utolewaji wa homoni nyingine iitwayo Gonadotropin-Releasing Hormaone-GnRH
kutoka kwenye sehemu ya ubongo.
Uwepo wa homoni ya GnRH husababisha pituitary gland kusababisha ongezeko la
homoni ya lutenizing (LH). Baadaye LH husababisha uachiliwaji wa yai kutoka
kwenye ovari, kitendo kinachojulikana kitaalamu kama ‘ovulation’.
Baada ya yai kutolewa kutoka kwenye ovari, husogezwa karibu na mfuko wa
uzazi ‘uterus’ kusubiri kuungana na mbegu za mwanamme, na endapo litakutana
nazo basi mimba hutungwa. Kama hakutatokea muunganiko kati ya yai na mbegu
(kitaalamu huitwa ‘fertilization’) basi yai humeguka na kufa ndani ya masaa 6
hadi 24.
Dalili za yai kutoka/kuachiliwa(Ovulation)
Muda mfupi kabla ya yai kuachiliwa kutoka kwenye ovari mwanamke hutokwa na ute katika mlango wa uzazi ambao huwa katika hali ya kuteleza na usio na rangi; ni kama sehemu ya nje ya yai bichi (isiyokuwa kiini).
Muda mfupi kabla ya yai kuachiliwa kutoka kwenye ovari mwanamke hutokwa na ute katika mlango wa uzazi ambao huwa katika hali ya kuteleza na usio na rangi; ni kama sehemu ya nje ya yai bichi (isiyokuwa kiini).
Ute huu huvutika sana pia. Mwanamke anapokuwa katika hali hii huweza kupata
ujauzito iwapo atagusana na mbegu za kiume. Ute huu husaidia kurutubisha mbegu
za kiume pindi zinaposafiri kupita mlango wa uzazi ‘cervix’.
Iwapo mwanamke hayupo katika kipindi hiki cha yai kuachiliwa, ute wa kwenye
mlango wa uzazi ‘cervical mucus’ huwa na rangi tofauti na katika hali ya
tofauti.
Ute huu huweza kuwa unanata, mweupe kama maziwa, ukiwa na muonekano kama
losheni ya kujipaka au kuwa na rangi ya njano. Ute huu huwa hauvutiki na huwa
na harufu kali kidogo.
Aidha, nafasi ya mlango wa uzazi nayo hubadilika wakati wote wa mzunguko wa
hedhi. Wakati wa yai kuachiliwa kutoka kwenye ovari, mlango wa uzazi husogea
juu kidogo na njia hutanuka kidogo zaidi. Baadhi ya wanawake huhisi hali ya
maumivu wakati wa yai kuachiliwa.
Maumivu haya hutofautiana na huweza kuwa ya kuvuta au ya jumla katika
sehemu ya tumbo, au maumivu ya kukata upande mmoja wa tumbo ambao ndio yai
huachiliwa
.
Ni siku gani yai huachiliwa (ovulation)?
Mara nyingi wanawake huamini kuwa yai huachiliwa katikati ya mzunguko wa
hedhi. Ukweli ni kwamba yai huachiliwa siku 12 hadi 16 Tokea mzunguko kuanza
Kwahiyo, japokuwa kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28 yai lake laweza
kuachiliwa katikati ya hedhi (kati ya siku ya 12 na 16), mwanamke mwenye
mzunguko wa hedhi wenye siku 36 yai lake huachiliwa kati ya siku 16 na 22.
Kwa wanawake wenye mizinguko isiyobadilika sana, njia nzuri ya kukadiria
siku ya yai kuachiliwa ni kutoa 16 kutoka kwenye jumla ya siku za mzunguko wake
wote na baada ya kupata jibu, ajumlishe jawabu hilo na 4. Hii itampa siku ambayo
yai huweza kuachiliwa.
Kwa mfano, mwanamke mwenye mzunguko wenye siku 22 mara nyingi yai lake
huachiliwa kati ya siku ya 6 hadi 10 ya mzunguko wake (22-16=6, halafu 6+4=10).
Siku
za hatari za mwanamke ni zipi?
Hizi ni
siku ambazo mwanamke akishiriki ngono bila kutumia kinga anapata ujauzito bila
wasiwasi wowote labda kama ana matatizo yanayomfanya asibebe mimba au mwanaume
wake ana matatizo.
Utazijuaje
siku hizo?
Kwanza
kabisa ili ujue siku zako za hatari lazima ujue idadi ya siku za mzunguko wako.
Kuna aina tatu za mzunguko.. mzunguko mrefu ambao unachukua siku 35, mzunguko
mfupi unaochukua siku 25 na ule wa kawaida unaochukua siku 28 na ndio mzunguko
ambao watu wengi wanao.
Baada ya
kujua siku amabyo yai linaachiliwa unaongeza siku 3 mbele na unatoa siku tatu
nyuma yaani mfano mzunguko wako ni siku 28 siku yai litakapoachiliwa ni siku ya
14 ukiongeza siku tatu mbele unapata 17 na ukitoa siku tatu nyuma unapata 11
hivyo siku za hatari inakua siku ya 11 hadi 17.
Kwa nini
tunaongeza siku 3 mbele? Ni kwamba yai pindi linapoachiliwa huweza kuishi siku
tatu tu baada ya hapo limekufa ndo maana ndani ya hizi siku tatu baada ya yai
kuachiliwa mbegu za kiume zikiingia mtu anapata mimba kwa sababu yai bado liko
hai.Na tunatoa siku tatu nyuma kwa sababu Mbegu za mwanaume pia huweza kushi
siku tatu tu,kwa hiyo mbegu zikiingia ndani ya siku hizi tatu kabla ya yai
kuachiliwa pindi yai litakapoachiliwa litakuta mbegu zipo hai.
Dalili
kwamba uko kwenye siku za hatari ni zipi?
Muda mfupi kabla ya yai kuachiliwa kutoka kwenye ovari mwanamke hutokwa na
ute katika mlango wa uzazi ambao huwa katika hali ya kuteleza na usio na rangi;
ni kama sehemu ya nje ya yai bichi (isiyokuwa kiini).Pia tumbo kuuma kidogo na
joto la mwili kuongezeka.


No comments