Leo ningependa nizungumzie namna gani unaweza ukaandaa/kutengeneza juice
yako ya matunda na mbogamboga ambayo hio juice inakuwa haijapoteza
ufanisi wake katika tiba mwilini mwetu.
Somo hili nimeliandaa hasa kwa madhumuni yafuatayo:
*Kutoa elimu kwa mwandaaji wa chakula cha familia kuwa chakula anacho andaa basi kiwe hakija poteza uhalisia kuwa tiba mwilini.
*Kufundisha jamii namna gani CHAKULA ASILI kinaweza kutumika kama tiba na kukuepusha na magonjwa mbali mbali.
*Kukufundisha namna gani unaweza kuandaa chakula chako asili ambacho
kitakusaidia kuondoa athari ya vyakula mbali mbali zinazopelekea kupata
magonjwa mbali mbali kama uzito kupita kiasi, kisukari,shinikizo la
damu, vichocheo vya kike kuvurugika nk
*Tutakupatia faida mbali mbali ya vyakula katika mlo wako wa kila siku.
Hivyo basi uandaaji wa chakula ambacho ni bora kwa afya yako inahitaji
elimu sahihi ili kuweza,kuwezesha mwili wako kurudisha na kuimarisha
utendaji kazi wake.
Kitu ambacho nataka nikwambie ni kuwa mfumo wa CHAKULA ni mfumo
unaounganisha mifumo mingine yote. Nina maana kuwa endapo mfumo huu
ukiathiriwa mifumo yote mingine ya mwili inavurugika ndio maana sasa
sisi kama wataalamu wa vyakula na waandaji wa kipindi hiki tumeona ni
jukumu letu kukupa msaada huu kuhakikisha tunaimarisha mfumo wako wa
chakula katika utendaji kazi wako.
Basi leo tujifunze NAMNA YA KUANDAA JUICE YAKO SAFI KABISA NYUMBANI KWAKO YENYE FAIDA KIAFYA:
KWA NINI TUNAHITAJI JUISI?
*Unywaji wa juisi ya matunda na mboga mboga unatusaidia kupunguza
kiwango cha mboga mboga na matunda na kuyaweka katika glasi tu. Hivyo
badala ya kula mboga beseni zima unaweza kukamua ukapata glas mbili
ukanywa kama juisi.
*Kwa kawaida unashauriwa upate matunda na mboga mboga zaidi ya aina tatu
kwa kila mlo. Sasa kutokana na uchumi hatuwezi kuhakikisha hili
unatekeleza na hivyo tunakuwa tuna ishi na miili yetu iliyopungukiwa
vitamini na madini mbali mbali mwilini mwetu. Upungufu wa madini muhimu
mwilini km manganese, chuma na vitamini muhimu zinafanya mwili
kutotekeleza shughuli za mwili ipasavyo. Hivyo vitu navifananisha km
mbolea za mwili zinazofanya shughuli zote za mwili zienda ktk usawa
unaotakiwa. Kupungukiwa kwa matunda na mboga mboga kunasababisha mwili
kushindwa kuunguza mafuta mwilini vizuri, kushindwa kuondoa takamwili na
magonjwa mbali mbali ya kimwili.
kupitia unywaji wa juice UNAJIPATIA VITAMIN NA MADINI MENGI hii pia ni
nzuri zaidi kwa wale wavivu wasiopenda kula mboga na matunda kupitia
juice wataboresha miili yao na kupata madini yote na vitamini zote
* Juisi za matunda na mboga mboga zina sifa hizi kubwa kabisa,
~Hazina kabisa cholesteral(ziro cholesteral)
~Hazina mafuta
~Hazina sukari nyingi
~Zina madini mengi na vitamini nyingi.
~Zinaondoa athari zote za vyakula vya viwandani na kurudisha uwezo wa
mwili wako ku unguza mafuta mabaya yote na shuguli zote kufanyika
ipasavyo.
NAMNA YA KUANDAA JUISI YAKO KWA MLO WAKO WA NYUMBANI:
Baada sasa ya kujifunza kwa nini tunahitaji juisi miilini mwetu basi
tujifunze namna ya kutayarisha na kuandaa matunda na mboga mboga ili
uweze KUTENGENEZA JUISI NZURI KWA MATUMIZI YAKO YA NYUMBANI
MAHITAJI
~MBOGA ZA MAJANI
Mfano: Kabeji,spinach nk
~Matunda
Mfano: Ndizi, apple, chungwa nk
~Vionjo asili
mfano:Mdalasini, tangawizi , kitunguu swaumu. Nk
~Maji ya kuoshea
~Kisu
~Kikamua juisi (Juicer)
*Kama hizi ni mboga mboga au matunda umelima kwa kutumia mbolea na dawa
za viua wadudu asili nakushauru unaosha vizuri kisha unapunguza ukubwa
wa bonga zako au matunda kwa kutumia kisu chako na hakikisha vipande
hivyo vinaweza kuingia vizuri kwenye blender yako
*Kama huna uhakika na matunda hayo ulimwaji wake na hizo mboga mboga
.mfano kabeji unaweza kuondoa kwanza yale maganda ya juu ili kuepusha
kukamua juisi yenye viambata vya viua wadudu(chemical pesticides). Hivyo
itakusaidia baada ya kuondoa maganda ya juu au layer ya juu basi osha
kwa maji mengi sana kuondoa hizo kemikali za dawa.
AINA YA VIFAA VYA KUKAMULIA JUISI
Watu wengi tumekuwa tukiitumia juisi kama vinywaji vingine tunavyotumia kwenye sehemu za starehe.
Hivyo basi LEO TUTAJIFUNZA MAAJABU YA JUICE ILIYOTENGEZWA KUFUATA
MASHARTI NA UKABORESHA AFYA YAKO UNAPOKUWA UNAPATA MLO WAKO WA KILA
SIKU.
Vifaa vya kutengenezea juisi vipo vya aina mbali mbali lakini katika
makala hii nitasema kwa ufupi kuhusu vifaa hivi vya kutengenezea juisi
zetu ili tuone kama ni salama kwa matumizi yetu:
1. CENTRI FUGAL JUICER
Hii ni aina ya kikamua juisi ambacho ndani kuna kifaa kinachozunguka kwa
kasi na kutoa sauti kwa nguvu. Aina hii ya kikamua juisi hutumika
kusaga juisi yako yote na pia ni kifaa ambacho hakipotezi uhalisia wa
nyuzi nyuzi za matunda yako.
Nyuzi nyuzi hizo hufanya tumbo la chakula kushinda kwa muda mrefu likiwa
limejaa na hivyo kutolewa kwa kichocheo cha leptin na seli zakuhifadhi
mafuta ambayo inaenda kwenye ubongo na kukata hamu ya chakula na
hatimaye kuzuia ulaji wa mara kwa mara ambao huchangia uchovyaji wa
insulin kwa wingi na kusababisha mafuta mengi kuhifadhiwa pamoja na
kuvurugika kwa vichocheo.
Hivyo ulaji wa matunda na mboga mboga zenye nyuzinyuzi (fiber) kwa wingi
ni muhimu sana kuondoa tatizo kwa wanao shinda wanakula mara kwa mara
na wale wanao taka kupunguza uzito.
**Hasara Za Kikamua Juisi Cha Centri Fugal**
Kile kibati kinazunguka kwa kasi sana hivyo huchemka na hatimaye
kuongeza joto na hewa ya oksijeni ambayo inaweza athiri viini
(Nutrients) mahususi vya juisi yako. Hivyo ili uweze kupata viini vyako
unapokuwa unatumia kikamua juisi hiki hakikisha kuwa unakunywa juisi
yako mara tu baada ya kuitengeneza au unaweza kuhifadhi kwenye kibebeo
ambacho kina mfuniko imara sehemu yenye giza au mwanga hafifi kwani
juisi huathiriwa na mwanga na hewa.
Ukikiuka utaratibu huo ni dhahiri kuwa juisi itakuwa haitumiki kama
tiba kiafya bali itakuwa kama kinywaji cha kwenye majumba ya starehe.
Kikamua Juisi hiki kinapokuwa kinazunguka kwa kasi kinapiga kelel sana
hivyo inaleta usumbufu kwani hakuna sehemu ya kupunguzia kelele.
Kumbuka kuwa vikamua juisi vya aina hii ndivyo vitumikavyo mara kwa
mara kwani vinauzwa kwa bei ya chini kidogo na kila mtanzania anaweza
kumiriki. Hivyo kama na wewe unatumia aina hii ya kikamua juisi fuata
masharti mazuri kabisa.
2. COLD PRESS JUICER
Hii ni aina ya kikamua juisi ambayo ina mfumo wa hali ya juu wa kukamua
juisi pia hutenga nyuzi nyuzi na kubakiza na juisi peke yake.
Pia aina hii ina uwezo mkubwa wa kutoa viini vyote vya lishe yani
Nutrients na pia utumiapo mashine hii utajipatia kiwango kingi cha juisi
kuliko ungetumia CENTRIFUGAL.
Kikamua juisi hiki hakipigi kelele kabisa na una uwezo wa kuihifadhi
juisi iliyo tengenezwa mashine hii kwa muda wa masaa 72 bila kuathiri
viini vya lishe; kwani haizalishi joto kama aina nyingine hivyo hulinda
sana viini vya tunda na mboga mboga.
Pia aina hii ya kikamua juisi ni nzuri sana kwa wale wanopenda kutumia
kupata juisi ya mboga za majani kama spinach, kabeji kwani ina uwezo wa
kusaga vizuri na kukupatia juisi iliyo sheheni viini vya lishe.
INA UWEZO WA KUKAMUA JUISI ZAIDI YA ASILIMIA 20-25 UKILINGANISHA NA AINA YA KWANZA
**™Hasara Za Kikamua Juisi Hiki**™
Inaondoa nyuzi nyuzi kwenye juisi yako na hivyo basi utumiapo juisi hii
tambua kuwa ni juisi ambayo ina nyuzi nyuzi kidogo sana na hivyo
inaweza kukufanya sukari yako iwe imepanda muda wote na kukufanya uzito
wako kuongezeka,kuchoka na mengine mengi.HIVYO SIO NZURI SANA KIAFYA
Ni gharama sana kuinunua kwani mtu mwenye kipato kidogo hawezi kumudu kuwa nayo.
Zingatia:
Tafiti zinasema kuwa juisi nzuri ni ile inayohifadhiwa katika chupa ya
kioo na sio chupa au galoni ya plastic. Hivyo ningependa wewe unaye taka
kuhifadhi juisi yako fuata masharti hayo ili uweze fikia malengo yako
kiafya.
No comments
Post a Comment