Mafua
ni moja ya magonjwa ya mfumo wa hewa ambayo mara kwa mara huwapata watoto wa
chini mitano. Mafua huweza kuwapa watoto mara 5-10 kwa mwaka mmoja.
Watoto
wa chini ya mwaka mmoja wakiwa na mafua huwa katika hali ngumu kwani kushikwa
kunyonya vizuri. Wazazi huwa na hofu sana pale wanapoona watoto wanapokuwa katika hali ya mafua na kikohozi.
Kama
hatua ya haraka hazitachukuliwa mwanzoni hapo baadae huwa ni makaribisho mazuri
kwa ugonjwa hatari wa homa ya mapafu maarufu kama Nimonia.
Si kila
kikohozi au mafua yanahitaji kupewa dawa na si sahihi kujinunulia dawa au
kuandikiwa na mtu asiye daktari. Hatari ya kutumia kiholela dawa zake ni pamoja
na kujitokeza kwa usugu wa bakteria dhidi ya dawa, kushusha kinga ya mwili na
kuharisha.
Zaidi
ya asilimia 80 ya mafua ya kawaida husababishwa na virusi ambavyo hakuna dawa
ya kuwauwa. Hupona yenyewe ndani ya wiki moja. Virusi hawa ambao hushambulia
tando laini za mifereji ya pua na kooni.
Mara
zingine virusi wa mafua huweza kuenea katika mfumo mzima na kuenea katika
mirija ya hewa kusababisha shambulizi la mirija ya hewa. Inaweza kushambulia
tishu za mapafu na kusababisha homa ya mapafu. Ugonjwa unaongoza kusababisha
vifo vya watoto chini ya miaka mitono duniani.
Mafua
pia husababishwa na mzio, kuvuta hewa chafu yenye vumbi, moshi inayokereketa
kama wenye kemikali za sumu na hali ya hewa ya baridi na unyevu. Dalili za
mafua na kikohozi kisichozidi wiki mbili, mikoromo wakati ya kupumua, kupiga
chafya, pua kuchuruzika maji maji au kamasi.
Kamasi
ikiwa haina rangi, yaani hali ya umajimaji inakuwa imesababishwa na virusi
wakati ikiwa ya njano au kijani inakuwa imesababishwa na bakteria. Dalili
zingine ni joto la mwili kupanda, kushindwa kunyonya na kupumua vizuri, kulia
na kutokuwa mtulivu.
Watoto
wanaonyonya waendelee kunyonyeshwa kipindi chote cha ugonjwa kwani maziwa ya
mama kiasilia huwa na lishe yenye kinga inayomlinda dhidi ya magonjwa. Mtoto
ambaye ameanza kutumia chakula cha kawaida ni vyema ukatumia vitu kama chai na
ukaidondoshea matone ya limao au machungwa.
Machungwa,
limao na ndimu huwa na vitamin C inayosaidia kufupisha dalili za mafua.
Hakikisha pia unampatia maji ya kunywa ua kutosha yasiyo baridi kwa ajili ya
kuurudishia maji mwili. Ni vyema kutumia maji ya moto kumuogesha na kumkinga na
baridi kwa kumvisha nguo zakutanda mwili mzima.




No comments
Post a Comment