Ni vyema tuelimishane kupitia blog hii ili sote
tuwe na tahadhari ya aina fulani hasa kuhusiana na magonjwa haya ya
kujitakia, ndio ni ya kujitakia, yanaitwa Lifestyle Diseases ama
magonjwa yasababishwayo na mitindo yetu ya maisha.
"What you eat may play a role in your risk of colon cancer. Colon cancer
may be associated with a high-fat, low-fiber diet and red meat.
However, some studies have found that the risk does not drop if you
switch to a high-fiber diet, so this link is not yet clear.
Smoking cigarettes and drinking alcohol are other risk factors for
colorectal cancer." kwa mujibu wa U.S National Library of Medicine
Ndio maana nikasema ni ya kujitakia, tafiti zaonesha "90% of chronic diseases come from infection of gastrointestinal"
na sababu kuu ni tatizo la kukosa choo, mi nilikuwa najiona sawa tu kama
sijaenda haja siku moja au mbili, nikidhani ni kawaida, kumbe nilikuwa
nalundika matatizo, mtu yeyote ambaye anapata mlo walau mlo mmoja kwa
siku na kupitisha siku moja au zaidi bila kupata choo anatatizo la
kukosa choo, sasa je weye unaye pata milo mitatu kwa siku bila kutoa
uchafu huo je wadhani waenda wapi? kitaalumu tatizo hili lajulikana kama
Constipation.
Wataalamu wanasema sababu ziko nyingi ikiwa ni pamoja na:-
Kukosa mlo kamili ama kula vyakula viingi vyenye kiwango kikubwa cha wanga na mafuta,
Kula vyakula vilivyokobolewa na vilivyo changanywa na madawa ili visiharibike,
mifumo hatarishi ya maisha (Dangeraous Lifestyles) kama vile matumizi ya pombe na sigara kwa wingi,
Ukosefu wa kiwango cha kutosha cha mbogamboga na matunda katika milo yetu,
Maji yasiyo salama,
Kuvuta hewa chafu,
Hizi ni baadhi tu, na hadhari zake zaweza kuwa:-
Chakula kutomeng'enywa vizuri (poor function of digestion system)
Maumivi makali wakati wa kupata choo,
Uchafu uliokaa muda mrefu kugeuka sumu,
Bakteria wenye madhara kuzaliwa na kuathiri utumbo mpana na viungo vingine mwilini.
Hii yaweza sababisha magonjwa sugu kama:
Saratani ya utumbo mpana (Colon Cancer)
Presha (Arteriosclerisis)
Kuongezeka uzito (Obesity)
Tumbo kujaa gesi
Magonjwa ya Ini
Figo kushindwa kufanya kazi vizuri,
Magonjwa ya ngozi,
Kukakamaa kwa mishipa ya damu,
Kisukari,
Magonjwa ya moyo n.k



No comments
Post a Comment