Sunday, 23 April 2017

TANGAZO: HUDUMA YA UPASUAJI KWA WATOTO WENYE ULEMAVU WA VIUNGO

Ndugu Wakapuchini(Watawa wa Shirika la Mt. Francisco wa Asisi) Kituo cha watoto walemavu Mlali Dodoma (Mlali Rehabilitation Centre) wanatangaza huduma ya upasuaji kwa watoto wenye ulemavu wa viungo.
Madaktari kwa ajili ya upasuaji wa watoto watatoa huduma hii katika Kituo chetu cha Mlali kuanzia tarehe 19-28/05/2017. Naomba uwatangazie ndugu, jamaa na wengineo habari hii, ili akiwepo mwenye kuhitaji huduma hii aweze kujiandaa na kuipata kwa wakati. Tafadhali wasiliana na wahusika kwa namba za simu zilizoko hapa chini.
Watoto watakaochekiwa ni wenye umri kati ya miaka 2 hadi 13, na ni wale wenye matatizo ya viungo.


Namba za mawasiliano ni hizi:
Mkurugenzi - 0754 876 333 na 0784 613 898
Msaidizi - 0755 745 438 na 0629 245 015
Sr Norine 0762 389 686 na 0754 097 520
Mtaalam wa mazoezi ya watoto 0769 441 943
*Forward kwa wengine huenda tukamsaidie mtoto mmoja ama zaidi.*

No comments

Post a Comment