Thursday, 20 April 2017

MATUMIZI YA DAWA ZA KIENYEJI SAMBAMBA NA DAWA ZA HOSPITALINI



Ndugu wapenzi na wafuatiliaji wa taarifa mbalimbali za mambo ya afya kupitia Blog yenu yaDOCTOR JOH, ni matumaini yetu kuwa nyote mpo katika hali nzuri kiafya kwa uwezo wa muumba wetu.
Katika changamoto tunayopenda kuwashirikisha na kuwaomba mtoe maoni yenu siku ya leo, ni changamoto inayohusu matumizi ya dawa za kienyeji sambamba na dawa za hospitalini. Jambo hili ni miongoni mwa mambo ambayo yanatokea kila siku katika maswala yanayohusiana na afya, mgonjwa anapelekwa hospitalini, kulingana na hali yake Daktari anaona ni vyema mgonjwa alazwe ili apate uangalizi wa karibu kutoka kwa wataalamu wa afya, wakati mgonjwa anaendelea kupewa huduma hospitalini, inagundulika kuwa anatumia pia dawa za kienyeji ili kujitibu. Matumizi haya ya dawa za kienyeji sambamba na dawa za hospitalini yanatokea majumbani kwetu pia. Je, kwa mtazamo wako jambo hili unalionaje?.

No comments

Post a Comment