Watu kwa mamia huvunjika miguu kote duniani kila siku kutokana na ajali mbalimbali hasa zinazohusisha usafiri kama magari na pikipiki. Wengine huvunjika wakiwa kazini na hata majumbani. Wote hawa wanahitaji kuunganishwa mifupa yao ili wapone na kuendelea na maisha.
Kuunga kwa mifupa iliyovunjika huchukua muda mrefu na hivyo kuwafanya watu waugue kwa kipindi kirefu na kushindwa kuendelea na kazi zao. Lakini kuna mbinu za kusaidia kuharakisha kuunga kwa mifupa iliyovunjika ambazo zikifuatwa zitasaidia watu kupona kwa haraka.
Kwa ujumla uungaji wa mifupa inategemea sana umri wa mgonjwa na ulaji wake wa chakula chenye virutubisho muhimu. Mchanganyiko sahihi wa madini,vitamini na protini ni jambo la msingi kuzingatiwa.
Mambo 8 Muhimu Kuharakisha Kuunga kwa Mifupa Ilivyovunjika
-
Madini ya Kalisiam (Calcium)
Ila ifahamike madini haya pekee hayatoshi,ni lazima kuwepo na vitu vingine kama vinavyoelezwa hapa chini
Vyakula Vyenye Kalsiam Kwa Wingi:
- Mziwa na mtindi
- Soya
- Mboga za majani
-
Vitamini Muhimu toka Katika Mlo Kamili
Vitamini D ,C na K zinahitajika kwa wingi kuharakisha kuunga kwa mifupa iliyovunjika.
Vitamini D:
Upungufu wa vitamini hii inafanya kalsiam isifike sehemu inayohitajika toka katika damu.
Vitamini D inasaidia kunyonywa kwa kalsiam toka katika damu na kuelekezwa katika mifupa iliyovunjika ili kusaidia uungaji.
Vyakula Vyenye Vitamini D kwa Wingi:
- Samaki au mafuta ya samaki
- Kiini cha mayai
- Bidhaa za maziwa
Vitamini K:
Vitamini K inasaidia kuimarisha protini aina ya osteocalcin ambayo ni sehemu ya muundo wa mfupa. Vitamini K huifanya protini hii kuwa nzito na ngumu na hivyo kusaidia kuimarisha mfupa unaoounga.
Vyakula Vyenye Vitamini K kwa Wingi:
- Mboga za majani
- kauliflawa
- Samaki
- Mayai
Vitamini C:
Vitamini C inasaidia kupona kwa mifupa iliyovunjika. Vitamini C kama inavyosaidia kupona kwa vidonda inasaidia pia kuunga kwa mifupa kwa kusaidia kuundwa kwa chembe za kolageni (collagen) ambazo zinatengeneza mifupa.
Vyakula Vyenye Vitamini C kwa Wingi:
- Machungwa na Ndimu
- Kabichi na Mboga za kijani
-
Kupunguza Matumizi ya Dawa za Maumivu
-
Kuacha Uvutaji wa Sigara
Lakini pia ni kwakuwa sigara inapunguza mzunguko wa damu mwilini kwa kufanya damu kuganda.
-
Zuia Vyakula Vinavyonyonya Mifupa
Vyakula hivivipunguzwe ilikuharakisha kuunga kwa mifupa iliyovunjika.
-
Kuongeza Ulaji wa Kalori(Wanga)
Mahitaji ya kawaida kwa mwanaume ni kalori 2500 na mwanamke wa umbo sawa ni kalori 2,000 tu.
-
Ulaji wa Protini kwa Wingi
- Kufanya Mazoezi
Kwa mgonjwa aliyevunjika hasa miguu huenda hili lisiwe jambo rahisi,lakini mazoezi yanaweza yakahusisha viungo ambavyo havijapata madhara ili mradi visaidie kufanya damu izunguke vizuri.
Mgonjwa anaweza kutembea hata kama anatumia magongo,au kufanya mazoezi akiwa amekaa ili mradi mzunguko wa damu uongezeke.
Mwisho
Kama wewe ni mgonjwa au una mgonjwa aliyevunjika basi njia hizi zitasaidia kuunga kwa mifupa iliyovunjika kwa haraka na kumfanya mgonjwa aendelee na shughuli zake za kawaida.Asante kwa kusoma mada hii na nakutakieni afya njema. Ukiwa na mawazo maoni au maswali shiriki nasi kwa kuandika katika kisnduku hapa chini.
Sambaza “Upendo” washirikishe unaowapenda na kuwajali,bonyeza SHARE hapo chini

No comments
Post a Comment