1.POTOFU: Kupiga mswaki mara nyingi na kwa nguvu huzuia kuoza kwa meno
UKWELI: Si mara ngapi unapiga mswaki na nguvu gani inatumika,
suala ni unapigaje mswaki. Kupiga mswaki mara nyingi na kwa maguvu
kunaweza kupelekea kukwangua sehemu ngumu ya nje ya jino, kulifanya
laini na hatimaye kuuma au hata kuvunjika.
Kupiga mswaki marambili, taratibu na kwa njia sahihi ndicho kinachosaidia meno kuwa na afya
2.POTOFU: Huna haja ya kumuona tabibu wamenokama hujaona au kuhisi una tatizo la meno.
UKWELI: Kila mtu anatakiwa kumuona tabibu wa meno angalau mara
mbili kwa mwaka bila kujali meno yake yanaonekana vizuri au imara kiasi
gani.
Si meno yote yanayo onekana mazuri na imara ni mazima, mengine yanaweza
kuwa yameoza katikamaeneo usiyoweza ona kama chini ya fizi na kwenye
mizizi, si hivyo tu hata uoto mpya(neoplasm)uweza kugundulika mapema
kabla ya kufanya uaribifu mkubwa kama utachunguzwa na wataalamu.
Kumbuka pia mangonjwa ya mifumo mingine kama ukimwi,kisukari na mengine
mengi hujidhihirisha mapema kinywani kabla mgonjwa hajapata dalili
zingine.
3.POTIFU:Usile kitu chochote unapo kwenda kung’oa jino
UKWELI:Njaa inaweza kukufanya uzirahi katika zoezi la kungoa
jino, hofu ikichanganyika na sukari kidogo mwilini husababisha ubongo
kushindwa kufanya kazi sawa sawa.
Imani hii potofu inahusishwa na sindano ya ganzi, watu wengi wanafikiri kila ganzi inatakiwa mtu awe hakula kwa muda fulani.
Hii kwa matibabu ya meno sio kweli kwani ganzi hutolewa kwenye eneo husika tu(local anaesthesia)hivyo haiathili mwili mzima.
4.POTOFU:Usitoe jino au kufanya matibabu ya mzizi wa jino kama una uvimbe hasa usaha
UKWELI:Kung’oa jino au matibabu ya mzizi wa jino yanasaidia kutoa
nafasi/njia kwa usaha kutoka na hivyo kupona haraka pengine bila hata
kuhitaji dawa(antibiotics).Yaweza kuwa kweli pale tu kama mgonjwa
atukuwa na homa au hawezi fungua kinywa ambapo itabidi udhibiti homa
kwanza, na kama ni kushindwa kufungua kinywa yabidi kuacha na kutibu
kinacho mfanya ashindwe kufungua kinywa kwanza.
5.POTOFU:Mama mjamzito hastahili kutoa jino mpaka atakapo jifungua
UKWELI:Kumuacha mama mjamzito na maumivu pamoja na ugonjwa
kwaweza kufanya ugonjwa kusambaa na kuingia kwenye ubongo hata kupelekea
kifo cha mama na kiumbe chake. Pia maumivu makali yaweza kusababisha
mimba kutoka.
6.POTOFU:Njia ya uhakika ya kutibu jino ni kuling’oa
UKWELI:Ziko njia nyingi na za uhakika za kutibu jino bila kungoa.
Kung’oa jino kama tiba ni pale tu ambapo jino hilo haliwezi tibika kwa
njia yeyote na kukaa kwake kwa weza kuleta madhara zaidi.
Kutoa jino huleta madhara mengine na meno bandia pamoja na kwamba
hayawezi kurejesha kazi za meno yaliyotoka kwa kiwango halisi, lakini
pia utunzaji wake ni mgumu na gharama pia. Hata hivyo kama umelazimika
kupoteza meno basi meno bandia ndilo chaguo pekee.
7.POTOFU:Kuweka dawa ya kutuliza maumivu kama aspirini kwenye tobo kunasaidia kutoa maumivu.
UKWELI:Kama ilivyo kwa magonjwa mengine, kutuliza maumivu wakati
kisababishi cha maumivu hakija shugulikiwa ni kulikuza tatizo kwa
gharama.Mbali na hivyo dawa kama aspirini uunguza fizi zilizozunguka
jino ulimoiweka, pia ulilainisha(weaken)na kufanya uotaji wake uwe mgumu
kwani uvunjika vunjika hovyo hovyo
8.POTOFU:Kutoa jino husababisha kifo
UKWELI:Kuendelea kukaa na jino lililooza na halifai kuzibwa
hufanya ugonjwa kusambaa na kusababisha kifo. Unaonekana kama ukweli
pale tu mgonjwa anakuja hospitalini kutoa jino
9.POTOFU:Meno mazuri urithishwa(inherited)
UKWELI: Eti kwa vile tu mama au baba ana meno mazuri na mazima na wewe utakuwa hivyo au kinyume chake.
Urithi unachangia kiasi kidogo sana, utunzaji wa meno vizuri na kukutana
na tabibu wa meno mara kwara ndio njia muhimu ya kuweka meno na kinywa
chako sawa.
10.POTOFU: Hakuna haja ya kuhangaika na meno ya utotoni kwani yatatoka baada ya muda wake kufika
UKWELI: Meno ya utotoni yasipotunzwa vizuri yanaweza kusababisha
kutoka/ kutolewa kabla ya muda wake na kupelekea meno ya ukubwani kuota
kwa mpangilio usiopendeza, lakini pia katika kipindi cha mchanganyiko wa
meno ya ukubwani na utotoni, meno ya utotoni yaliyooza yaweza ambukiza
ya ukubwani.
11.POTOFU: Maumivu ya meno yatajiishia yenyewe baada ya muda.
UKWELI:Kama jino limeoza haliwezi pona kwa namna yoyote mpaka
lipate tiba hata kama haliumi. Ukiendelea kulidharau ugonjwa unaweza
kusambaa mpaka maeneo mengine kama ubongo, kifuani na hatimaye
kusababisha kifo.
Angalizo:
Ni asilimia tano tu kati ya wagonjwa ambao tatizo la jino limesambaa hadi kwenye ubongo ndio huweza kupona..

No comments
Post a Comment