Mbali
ya kuwa ni chanzo kikuu cha Vitamin A, B6, C, ‘Potassium’, ‘Magnesium’
na virutubisho vingine kibao, tunda hili pia lina virutubisho vingine
vyenye uwezo wa kuamsha hisia za kimwili (Sex libido) na kuondoa matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction).KAMA VIAGRA
Wanasayansi
wanasema kuwa Tikitimaji lina virutubisho vinavyoweza kuleta mhemuko wa
kimwili kama mtu aliyemeza kidonge cha kuongeza nguvu za kiume cha
Viagra. Tunda hili limeonesha kulainisha vizuri mishipa ya damu na
kufanya mzunguruko wa damu mwilini kuwa mwepesi bila athari yoyote
mbaya.
Tikitimaji lina kirutubisho aina ya ‘arginine’, ambacho
huchochea uzalishaji wa ‘nitric oxide’ kwenye mishipa ya damu na hivyo
kuongeza nguvu za kiume kama ifanyavyo dawa ya Viagra.
HUIMARISHA MISULI
Vyakula
vyenye kiwango kingi cha madini aina ya ‘Potassium’ kama vile
Tikitimaji, huimarisha misuli ya mwili na huwafaa sana wanamichezo.
Ulaji wa kipande kimoja cha Tikitimaji baada ya kufanya mazoezi makali,
huondoa tatizo la kukaza kwa misuli ya miguu.
HUSAIDIA KUPUNGUZA UZITO WA MWILI
Tikitimaji lina kiwango kidogo sana cha kalori lakini lina kiwango kikubwa cha maji
HUIMARISHA KINGA YA MWILI
Kirutubisho
cha ‘arginine’ kilichomo kwenye Tikitimaji mbali ya baadhi ya kazi
zilizoainishwa hapo juu, pia huchochea kwa kiasi kikubwa uimarishaji wa
kinga ya mwili.
HUONDOA SUMU MWILINI
kuondoa ‘ammonia’ na sumu nyingine mwilini ambazo zinapozidi humfanya mtu kusikia uchovu na kusababisha ugonjwa wa ini na figo.
tunda
hili hufaa kuliwa na wagonjwa wa presha kwani hushusha shinikizo la juu
la damu, huongeza nuru ya macho, hutoa kinga kubwa dhidi ya magonjwa
nyemelezi yakiwemo yale hatari kama vile kansa ya matiti, kibofu cha
mkojo, mapafu na kansa ya tumbo.

No comments
Post a Comment