Saturday, 25 March 2017

FUNGUO TATU ZA KUPUNGUZA UZITO WAKO KWA KUBORESHA MLO


Kabla sijaongelea mada ya leo FIKIRIA HAYA MAMBO MAKUU MAWILI.
~Kila siku watu tunaumwa,kichwa,maumivu ya mifupa,maumivu ya hedhi nk. Ukienda hospitali daktari atakupa dawa ya maumivu au unanunua mwenyewe dawa kama Buscopan,diclofenac,paracentamol,diclopar nk. Dawa hizi ziko mahususi kuondoa dalili sio chanzo cha tatizo(Symptomatic relief) na imeandikwa uzinywe kwa ushauri wa daktari hii ikiwa na maana kuwa hii ni dawa pia ni sumu ikitumiwa ovyo.Kama hujalike page yangu bofya like kuna makala inakuja JINSI DICLOFENAC NA DAWA ZINGINE ZINAVYO ASILI UKUTA WA UTUMBO WAKO NA KUPELEKEA KUPATA MAGONJWA SUGU
USHAURI:Siku zote tafuta chanzo cha tatizo sio kutibu dalili
~Hivi ukijiuliza swali umeenda kwa daktari ukifika ukiwa unalalamika kusumbuliwa na mawazo na kukosa usingizi. Daktari atakuambia unaumwa MSONGO WA MAWAZO na kukupa dawa ya kuodoa hiyo depression kwa mfano ANTDEPRESANT AMITRYPTIRIN.. Sasa je ametibu kiini cha tatizo au dalili. Ni dhahiri kuwa dawa zetu zinatibu dalili sio kiini cha tatizo ndio mana leo hii kila ugonjwa daktari anakuambia hautibiki. Ni dhahiri kuwa magonjwa tabia YANATIBIKA kama ukifuata ushauri unaozingatia kuondoa kiini.

FUNGUO ZA MAFANIKIO KWA AFYA YAKO

1. KULA VYAKULA VYENYE SUKARI KIDOGO
2. KULA VYAKULA VYA NYUZINYUZI KWA WINGI
3. KULA VYAKULA VYA MAFUTA KIDOGO
Basi ningependa tujadili moja baada ya nyingine mpendwa msomaji wangu:
VYAKULA VYA SUKARI NYINGI
~Nimekuwa nikizungumza sana kuhusu vyakula vya sukari nyingi katika milo yetu ya kila siku. Vyakula kama mikate, bina kiwango kikubwa cha sukari hivyo vinasababisha mwili kuchovya Kichocheo cha insulin kwa wingi na hatimaye kusababisha kiwango cha insulin kwenye damu kupanda. Insulin ni kichocheo kizuri sana lakini kiwango cha juu husababisha yafuatayo:
~Kinahifadhi mafuta mwilini katika mfumo wa glycogen
~Kinakufanya uzeeke haraka
~Kinazuia kichocheo cha LEPTIN ambacho huenda kunasa kwenye vipokezi vya ubongo na kutoa taarifa kuwa umetosha na kula(yani kushiba). Kuzuiliwa kwa hiki kichocheo ndio mana watu wenye uzito mkubwa utakuta anakula sana jua ana insulin nyingi ambayo inazuia Leptin ambayo hutoa taarifa ya kutoshelezwa la mlo kuzuiliwa.
~Pia insulin kuwa juu kunafanya tatizo lako la uchovyaji vichocheo kuharibika.
WANAUME
~Kiwango kingi cha insulin kwenye damu husababisha uchovyaji wa Testosterone kuzuilika hivyo kusababisha mwanaume kukosa shauku,hamu,nguvu na hamasa ya kuelendelea na tendo la ndoa. Hivyo basi inasemekana kwamba walaji wa vyakula hivi vya sukari mara nyingi huwa wana kiwango kingi cha insulin kwenye damu ndio mana wana matatizo mengine ya nguvu za kiume na mengine Kama chunusi sugu,macho kushindwa kuona vizuri nk
WANAWAKE
~Ninapenda kusikitika kuwa ongezeko la dada zetu na mama zetu wenye matatizo ya uzazi kama fibroids,cancer,mizunguko mibovu na maumivu wakati wa hedhi. Sasa ningependa nikwambie nini chanzo na hatua za kuchukua. Ulapo vyakula vya sukari nyingi vinakufanya kiwango cha INSULIN kuongezeka kuja kusawazisha sukari hiyo mwilini. Kuongezeka kwa insulini kunafanya uchovyaji wa ESTROGEN KUWA JUU na kushusha kiwango cha PROGESTERONE. Hiki tunasema HORMONAL IMBALANCE. Kuongezeka kwa kichocheo hiki kunasababisha yafuatayo:
~Estrogen ni mbolea nzuri sana ya vimbe mbalimbali mwilini mwako yan ESTROGEN DEPENDANT TUMORS kama FIBROIDS uvimbe kwenye kizazi,Kansa ya titi au uvimbe wa titi,Kansa ya shingo ya kizazi nk. Ni dhahiri kuwa ni changamoto kubwa namna au njia rahisi ya kutibu hili tatizo ni kusawazisha kiwango cha hormone na kuondoa uvimbe kwa operation. Unapofanyiwa operation haimanishi chanzo cha tatizo ambalo ni kiwango cha juu cha hormoni kimerekebishwa. Mbolea itabaki pale pale na wagonjwa wengi wanaofanyiwa operation ya kuondoa kiuvimbe na kuacha kizazi(myomectomy) hurudia tena uvimbe huo baada ya muda mfupi. CHANZO NI KULA VYAKULA HIVI VISIVYO NA FAIDA MWILINI BALI NI KUJIONESHA UFAHARI WA PESA.
~Pia kwa dada zangu wenye maumivu makali ya hedhi ambayo hupelekea kupata kichefuchefu,tumbo kuuma,mgongo kuuma,kuharisha,msongo wa mawazo,kula sana,na kuchoka sana bila kusahau hasira sana. Hii ni kutokana na kiwango cha juu cha insulin ambacho kufanya kiwango cha estrogen kuwa juu na progesterone kushuka hivyo kupelekea maumivu hayo. Matibabu ya hili tatizo ni changamoto pia, Utumiapo dawa za maumivu kama DICLOFENAC,BUSCOPAN,IBUPROFEN utafiti unaonesha kuwa zinaweza kupelekea ukapata tatizo jingine sugu ambalo ni kali zaidi ya hilo mwanzo huitwa PREMENSTRAL DYSPHORIC DYNDROME. Maumivu huongeza muda wake na yanakuwa makali kadri siku zinavyo enda. Hivyo utumiapo hizo dawa huondoi tatizo bali unazidi kuongeza usugu wa tatizo. Tiba ni kujua na kuepuka vyakula vibaya vyenye sukari nyingi na kurekebisha mwenendo wa maisha yako
INAENDELEA UFUNGUO WA PILI.....BOFYA LIKE PAGE YANGU UENDELEE KUPATA MAKALA ZANGU ZA AFYA.

No comments

Post a Comment