Wednesday, 25 January 2017

MAPITIO YA BIDHAA:MAZIWA GANI UMPATIE MWANAO ANAPOKUWA NA UMRI CHINI YA MIEZI 6

Watu wengi tumekua tukijiuliza ni Infant feeding formula gani tutumie kwa watoto wetu,na wengi wetu tumekua tukikimbilia kutumia bidhaa za bei nafuu pasipo kujua madhara yake kwa watoto wetu.zipo brands nyingi kwa sasa zinazotengeneza maziwa (infant feeding formula) hivyo basi ni vyema kuwa makini na brands tunazotumia kuwalishia watoto wetu.Kuhakikisha zina virutubisho vyote muhimu kwa mtoto.
MUHIMU:Tukumbuke maziwa ya mama ni bora kuliko Infant feeding formulas..hivyo hakikisha unampatia mwanao maziwa ya mama tu akiwa na umri chini ya miezi 6.


Leo tuongelee kidogo baadhi ya infant feeding formula unayoweza kutumia kwa mwanao akiwa chini ya umri wa miezi 6. Nadhani umewahi kusikia kuhusu maziwa ya NAN,yapo katika aina tatu tofauti kulingana na umri.leo tutazungumzia Starter feeding (chini ya miezi 6) ambayo ni NAN OPTIPRO H1 GOLD.
Bidhaa hii unaweza kutumia kwa mwanao tokea amezaliwa hadi kufikia miezi sita.ni bidhaa nzuri ya kuanzia kwani imesheheni virutubisho vyote muhimu vinavyohitajika kumsaidia mtoto kukua vizuri na kuimarisha kinga ya mwili wake.Ni bidhaa ambayo haijarepotiwa kuwa na maudhi madogo madogo kama kuharisha kwa watoto.

Hizi ni aina za virutubisho vinavyopatikana ndani ya NAN OPTIPRO H1 GOLD

Jinsi ya kuandaa:katika picha ifatayo nimejaribu kuonesha jinsi gani unavyoweza kuandaa NAN OPTIPRO 1,Hakikisha unazingatia usafi wakati wa maandalizi ili kuepuka kumsababishia mwanao magonjwa ya tumbo.

Una maoni yoyote au swali lolote kuhusu Maziwa haya? usisite kushare nasi kwenye comment box hapo chini.



No comments

Post a Comment