Tatizo hili
huwatokea zaidi wanawake walio katika umri wa kuzaa. Viungo vya nje vya
uzazi vya mwanamke ambavyo huathirika na tatizo hili la uvimbe ni
mashavu ya uke Mashavu au
midomo ya uke kitaalamu huitwa 'labia majora' ambayo ni midomo ya nje ya
uke na 'labia minora' ambayo ni midomo ya ndani ya uke. Uvimbe huo utokea kwenye tezi ya batholin.
TEZI YA BATHOLIN NI NINI
Hizi ni tezi zisizoonekana zipo kkwenye mashavu ya uke sehemu ya chini karibu na tundu la uke.
Tezi hizi husaidia kuzalisha ute ili kuufanya uke kuwa na unyevunyevu muda wote.
Uvimbe katika viungo vya nje vya uke
hutokea tu au husababishwa na maambukizi. Uvimbe huu unaweza kuwa na
maumivu au usiwe na maumivu. Uvimbe unaweza kuwa mdogo au mkubwa
kutegemea na sehemu ulipo na muda tangu ulipoanza.
Mwanamke pia
anaweza kupata tatizo la midomo ya ndani ya uke ambayo hurefuka na
kujiona kama kero, hiyo ni hali ya kimaumbile na haina madhara.
AINA ZA UVIMBE
Uvimbe wa mashavu ya uke huwa unatokea kwenye tezi iitwayo 'Bartholin
gland'. Tezi hii huwa haionekani kwa macho na mojawapo ya kazi zake ni
kutoa majimaji ya kulainisha uke wakati wa tendo la kujamiiana.
'Bartholin cyst', huu ni uvimbe mgumu hutokea pembeni ya shavu la uke
kwa ndani. Uvimbe huu mara nyingi huwa hauumi lakini huendelea kukua na
kuleta shida wakati wa tendo la kujamiiana, na hutokea tu wenyewe.
Uvimbe huonekana kwa macho au mwanamke anauhisi anaponawa ukeni au
wakati wa kujamiiana. Uchunguzi wa kina hufanyika ili kuangalia uhusiano
wake na sehemu nyingine za mwili. Matibabu ya aina hii ya uvimbe ni
upasuaji wa kuondoa kabisa.
'Bartholin Abscess'. Aina hii ya uvimbe
ni jipu kwani ndani yake huwa kuna usaha. Uvimbe huu huwa na maumivu
makali sana, hutokea upande mmoja wa shavu la uke. Mgonjwa pamoja na
kuwa na maumivu makali huweza kupata homa, kushindwa kutembea vizuri na
wakati mwingine uvimbe hupasuka. Maumivu husababisha mgonjwa ashindwe
kuendelea na mambo yake.
Matibabu ya uvimbe huu ni upasuaji na
kuondoa usaha wote kisha kurekebisha kingo za kidonda kitaalamu, hili
lisipofanyika, jipu hili huwa na tabia ya kujirudia rudia.
Athari ya
aina hii ya uvimbe ambayo ni jipu ni maumivu makali, kushindwa kufanya
tendo la ndoa na uvimbe unapasuka na kusababisha kidonda.
Uchunguzi na tiba yake hufanyika kwa Daktari bingwa wa kinamama kwenye Hospitali ya mkoa.
Uvimbe kwenye mdomo wa kizazi 'Cervix' huwa wa aina tofauti, uvimbe huu tutakuja kuuzungumzia kwa undani katika makala zijazo.
Dalili za matatizo katika mlango wa kizazi ni uvimbe katika mdomo wa
kizazi ambapo mgonjwa atauhisi wakati wa kujisafisha ambapo atahisi kitu
kama gololi katika mdomo wa kizazi kimeshuka chini.
Mwanamke pia
hulalamika maumivu wakati na baada ya tendo la kujamiiana, kutokwa na
uchafu ukeni mara kwa mara unaoambatana na muwasho na harufu mbaya
ukeni.
Wakati mwingine damu hutoka ukeni baada ya tendo au kuhisi kitu kinasukumwa kwa ndani wakati wa tendo la kujamiiana.
USHAURI
Ni vema uwahi Hospitali kwa uchunguzi na tiba, kama tulivyoeleza,
uchunguzi wa matatizo haya hufanyika katika Hospitali za mikoa kwenye
Kliniki za Madaktari bingwa wa magonjwa ya akinamama.
Hujatuambia ninichanzo kinachosababisha na matibabu yake yanagarim sh ngapi
ReplyDeleteMm nimemuelewa kasema inatokea tu kulingana na hormone so may b shida ya hormone imbalance ndo inasababisha tatizo
DeleteMatibabu yake ni nini zaidi ya upasuaji?.
ReplyDeleteMi niko na hiyo shida,sijaolewa na sikua najua kama ni kitu hutokea,na nimekua nikimficha mpenzi wangu,tezi hiyo ukiifinya yapotea halafu irudi,sasa kando na upasuaji kuna njia ingine yoyote ya kuitoa
ReplyDelete